Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Crawford dakika za jioooni kwa Madrimov

Muktasari:

  • Crawford alikuwa na rekodi bora ya kuwaangusha mabondia tisa tofauti waliokutana na kichapo chake hadi kushindwa kumaliza raundi zote, iliyoshindwa kufua dafu mbele ya Madrimov aliyempa ugumu kiasi chake Jumamosi iliyopita.

PAMBANO lililopita la bondia Terence Crawford dhidi ya Israel Madrimov lilikuwa la kwanza kwa Crawford kushindwa kumwangusha mpinzani wake, baada ya kumaliza raundi zote na kushinda kwa pointi za majaji.

Crawford alikuwa na rekodi bora ya kuwaangusha mabondia tisa tofauti waliokutana na kichapo chake hadi kushindwa kumaliza raundi zote, iliyoshindwa kufua dafu mbele ya Madrimov aliyempa ugumu kiasi chake Jumamosi iliyopita.

Hata hivyo, Crawford 'Bud' alishinda pambano la kwanza kwenye uzito wa Super Welterweight na kumvua mwenye mkanda Israel Madrimov ambaye hata hivyo hakuridhika sana na kichapo hicho kiasi cha kudai anastahili pambano la marudiano dhidi ya Crawford.

Mkanda huo sasa unampa rekodi bora Crawford ya kushinda mikanda ya uzito tofauti minne alisimika rekodi kali ya kushinda mapambano yote 41 aliyopigana bila sare wala kichapo tangu aanze kupanda ulingoni.