Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yamtangaza kocha mpya Rosenior

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo mwenye umri wa miaka 41 amefanya uamuzi mkubwa wa kuondoka katika klabu dada ya Ufaransa, Strasbourg, kufuatia kuondoka kwa kushangaza kwa Enzo Maresca siku ya Mwaka Mpya.

LONDON, ENGLAND: LIAM ROSENIOR ametangazwa rasmi kocha mkuu mpya wa Chelsea chini ya uongozi wa bilionea Todd Boehly na washirika wake.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 41 amefanya uamuzi mkubwa wa kuondoka katika klabu dada ya Ufaransa, Strasbourg, kufuatia kuondoka kwa kushangaza kwa Enzo Maresca siku ya Mwaka Mpya.

Viongozi wa klabu waliamua kuwa Rosenior, ambaye aliwahi kucheza katika klabu za Fulham, Reading na Brighton, ndiye mtu sahihi wa kuendeleza falsafa yao tata ya soka na sera ya usajili, kufuatia mafanikio yake katika Ligue 1.

CHEL 01

Chelsea ilisema ina “furaha kubwa” kumtambulisha Rosenior, ambaye amesaini mkataba mnono wa miaka sita na nusu.

Rosenior anatarajiwa kuwepo Craven Cottage, Jumatano kuangalia timu yake mpya ikicheza dhidi ya Fulham, kabla ya kuchukua rasmi mikoba ya ukocha katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Charlton, Jumamosi.

Taarifa ya Chelsea ilisema: “Rosenior anawasili Stamford Bridge baada ya kufanya kazi ya ukocha nje ya nchi akiwa na RC Strasbourg, ambapo aliiongoza klabu hiyo ya Ufaransa kufuzu mashindano ya Ulaya kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 19 katika msimu wake wa kwanza. Hii ni baada ya kuwa na majukumu ya awali England akiwa na Hull City na Derby County.

CHEL 02

“Liam ameonyesha kuwa ana uwezo wa kujenga timu yenye mtindo wa wazi wa uchezaji huku akiweka viwango vya juu zaidi kwa wachezaji ndani na nje ya uwanja. “Ingawa kutakuwa na msisitizo endelevu katika maendeleo ya wachezaji, matarajio na malengo ya klabu yanaendelea kuwa makubwa.

“Liam ana uwezo wa kutoa kiwango bora kutoka kwa kikosi hiki kwa haraka, na anajiunga nasi akiwa na jukumu pamoja na sapoti kamili kuhakikisha Chelsea inaendelea kushindana katika kiwango cha juu katika mashindano yote msimu huu na misimu ijayo. Karibu Chelsea, Liam!”

Makocah wengine waliotajwa kuwa kwenye orodha walikuwa Cesc Fabregas wa Como, Andoni Iraola wa Bournemouth, na aliyekuwa kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez.

CHEL 03

Hata hivyo, Rosenior aliwaacha viongozi wa Chelsea wakiwa wamevutiwa na dhamira yake ya kukuza vipaji vya vijana pamoja na uelewa wake wa mkakati wao wa kusajili wachezaji wengi na kujenga kikosi kipya.

Kocha huyo mpya amesema: “Nimejawa na unyenyekevu na heshima kubwa kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa Chelsea Football Club.

“Hii ni klabu yenye roho ya kipekee na historia ya kujivunia ya kushinda mataji.

“Kazi yangu ni kulinda utambulisho huo na kujenga timu itakayodhihirisha maadili haya katika kila mchezo tunaocheza, huku tukiendelea kushinda mataji.”