Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea, Liverpool zamgombea mtoto wa Robinho

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Ligi Kuu England inawania saini ya mshambuliaji huyo kinda baada ya kuonyesha kiwango bora akiibukia kikosini Santos.

SAO PAULO, BRAZIL: LIVERPOOL na Chelsea zimeripotiwa kuchuana jino kwa jino kwenye mchakamchaka wa kusaka huduma ya Robinho Jnr, 17 ambaye ni mtoto wa staa wa zamani wa Brazil, Robinho.

Miamba hiyo ya Ligi Kuu England inawania saini ya mshambuliaji huyo kinda baada ya kuonyesha kiwango bora akiibukia kikosini Santos.

Klabu hiyo maarufu ya huko Brazil, Santos ndiyo iliyowaibua wachezaji mahiri wa Kibrazili kama Pele, Rodrygo na Neymar, ambaye kwa sasa amerejea kuitumikia timu yake hiyo ya ujanani.

Ripoti zinafichua kwamba skauti wa Anfield, akiwamo msaka vipaji wa miaka mingi wa klabu hiyo, Dassler Marques, amekuwa mhudhuriaji mzuri sana wa mechi za Santos mwaka huu akienda kumtazama Robinho Jnr.

Licha ya kwamba kinda huyo bado hajaanza kupewa dakika za kutosha ndani ya uwanja, lakini Liverpool imekuwa ikimfuatilia kwa karibu sana.

Kinda huyo ameripotiwa kwa sasa anasimamiwa kupaji chake kwa karibu sana na Neymar, baada ya supastaa huyo wa zamani Barcelona, PSG na Al-Hilal kurudi kucheza soka lake huko Brazil.

Akivaa jezi maarufu iliyokuwa ikivaliwa na baba yake, Namba 7, Robinho Jnr anatazamwa kama mmoja wa mastaa wakubwa wa kizazi cha baadaye kwenye soka na ndiyo maana Liverpool na Chelsea zinahaha kumsajili.

Timu ya maskauti wa Chelsea huko Amerika Kusini, ikiongozwa na bosi wa zamani wa usajili wa klabu ya Corinthians, Alysson Marins, wamekuwa wakimfuatilia sana mtoto huyo wa Robinho, aliyewahi kuzichezea Real Madrid na Manchester City.

Chelsea haipo tayari kupoteza fursa ya kunasa saini ya kinda huyo ambaye amekuwa gumzo kwelikweli huko Brazil.

Chelsea imekuwa na mafanikio makubwa kwa kipindi cha karibuni kwa dili ilizofanya huko Brazil ikiwamo kumsajili, Estevao, ambaye amekuwa moto kwenye Ligi Kuu England.

Wanataka kufanya hivyo pia kwa Robinho Jr ili akaungane na Estevao huko Stamford Bridge.

Robinho, baba yake Robinho Jr kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka tisa jela baada ya kukutwa na hatia ya ubakaji katika tukio linaloripotiwa alilifanya 2013.

Mama yake, Robinho Jr, kwa sasa ndiye anayesimama kama wakala wa mchezaji huyo huku kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachohitaji ilipwe Pauni 43 milioni kwa timu itakayohitaji saini yake.