Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno Fernandes akataa kichaka cha Europa

BRUNO Pict

Muktasari:

  • Kikosi cha Ruben Amorim kipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England huku kikiwa na mechi nne zilizosalia ambazo hata ikishinda zote hazitoondoa rekodi ya kufanya vibaya msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes anaamini kushinda Europa League hakutobadilisha ukweli, msimu huu kwao ulikuwa ni mbaya.

Kikosi cha Ruben Amorim kipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England huku kikiwa na mechi nne zilizosalia ambazo hata ikishinda zote hazitoondoa rekodi ya kufanya vibaya msimu huu.

Hata hivyo, bado wana nafasi ya kugeuza hali hiyo kwa kushinda taji la Ulaya na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Lakini kabla ya mechi ya nusu fainali ya mkondo wa kwanza dhidi ya Athletic Bilbao itakayopigwa Alhamisi ya wiki hii, Bruno alisema mafanikio hayo hayataficha hali halisi ya msimu.

Kiungo huyo raia wa Ureno alisema: "Sidhani kama ni zawadi, nafikiri tutakuwa tumefanikiwa kwa kiwango cha Europa League pekee. Ni muhimu sana kufanya hivyo, kushinda kombe msimu huu. Lakini haitabadilisha chochote."

Bilbao wako nafasi ya nne kwenye La Liga na wana sababu ya ziada kutaka kufika fainali kwani mchezo wa fainali wa mashindano hayo utapigwa katika Mji wao mwezi ujao.

"Itakuwa mechi ngumu. Lazima tuwe tayari.”

Manchester United walinusurika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Bournemouth siku ya Jumapili baada ya Rasmus Hojlund kufunga bao katika dakika ya 96.