Bronny aanza mambo Lakers

Muktasari:
- Bronny akiwa pamoja na kinda mwenzake, Dalton Knecht walioingia kwenye drafti la mwaka huu kama namba 17 na 55 mtawalia, wameuwasha moto kwenye mchezo dhidi ya Cavaliers ambapo Knecht aliongoza kwa pointi 20 na ribaundi saba wakati Bronny alifunga pointi 13.
BRONNY James, mtoto wa supastaa wa NBA anayekipifa Losa Angeles Lakers, LeBron James, ameanza kuzima kelele za baadhi ya waliokuwa wanaponda kuhusu uwezo wake kama ataweza kucheza na kung’ara katika ligi hiyo kufuatia kufanya vyema katika mechi mbili mfululizo hususan mchezo wa juzi Ijumaa dhidi ya Clevaland Cavaliers.
Bronny akiwa pamoja na kinda mwenzake, Dalton Knecht walioingia kwenye drafti la mwaka huu kama namba 17 na 55 mtawalia, wameuwasha moto kwenye mchezo dhidi ya Cavaliers ambapo Knecht aliongoza kwa pointi 20 na ribaundi saba wakati Bronny alifunga pointi 13.
Mbali na mchezo wa mwisho wa kirafiki waliocheza jana dhidi ya Chicago Bulls, imeonyesha wazi kuwa timu hiyo chini ya kocha Jonathan Clay ‘JJ’ Redick wana kitu cha kupata kupitia ingizo la makinda hao wawili ambao wanaandaliwa kuitumikia timu hiyo misimu ijayo.