Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Boss Chelsea afunguka timu hiyo kuhama Stamford Bridge

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni The Blues itaondoka kwenye uwanja huo na itacheza kwenye uwanja mpya kwa miongo miwili. Mpango ni kujengwa uwanja mpya utakaokuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wanaoketi na utagharimu Pauni 500 milioni.

LONDON, ENGLAND: BILIONEA mmiliki wa klabu ya Chelsea, Todd Boehly amethibitisha klabu hiyo itaondoka Stamford Bridge na kuhamia kwenye uwanja mpya.

Kinachoelezwa ni The Blues itaondoka kwenye uwanja huo na itacheza kwenye uwanja mpya kwa miongo miwili. Mpango ni kujengwa uwanja mpya utakaokuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wanaoketi na utagharimu Pauni 500 milioni.

Mpango wa kuendeleza uwanjani huo ulithibitishwa mwaka 2015 wakati ikiwa chini ya bilionea wa Russia, Roman Abramovich, lakini mpango ulikuja kuvurugwa miaka mitatu baadaye.

Lakini, sasa tajiri mpya wa timu hiyo, bilionea wa Marekani, Boehly ameshapata eneo jipya la timu itakapokwenda kucheza huko Earls Court. Chelsea itaondoka Stamford Bridge, mahali ambako imekuwa ikipatumia kama uwanja wao wa nyumbani tangu mwaka 1905.

Boehly alisema: “Nadhani tumekuwa tukilifikiria hili kwa muda mrefu na sasa tunataka kulitekeleza. Tuna uwanja mkubwa wa kuufanyia maendeleo hivyo ni lazima tuufanyie kazi.”

Tajiri huyo aliongeza: “Kuendeleza viwanja ni kitu kinachochukua umaarufu kwa sasa. Miundombinu ya kimichezo, hilo lipo kwenye mipango yetu. Tuna miaka 16 hadi 20 ya kulitimiza hilo.”

Hivi karibuni, Manchester United ilitangaza mpango wao wa kujenga uwanja mpya wa Pauni 2 bilioni, utakaokuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 100,000.

Kwenye mpango wao Man United iliahidi itaboresha makazi ya watu yanayozunguka uwanja wa Old Trafford kitu ambacho kimeungwa mkono na serikali. Kuhamia Earls Court, Chelsea nayo inaweza kunufaika na mpango huo.

Ulipo uwanja wa Stamford Bridge ni pagumu kupanua, wakati sasa ukishika namba tisa kwa ukubwa kwenye viwanja wa Ligi Kuu England. Mpango wa kuondoka Stamford Bridge umekubalika na wamiliki wa sehemu ya kuchezea ya uwanja huo.