Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi Man United ataka kupunguza wengine

Muktasari:

  • Man United tayari imepunguza wafanyakazi 450 tangu Ratcliffe aliponunua hisa ikiwamo na kuvunja mkataba wa kocha wa zamani wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson, aliyekuwa balozi wa klabu.

MANCHESTER, ENGLAND: TAJIRI wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe anatarajiwa kumfuta kazi ofisa wa muda mrefu wa timu hiyo ikiwa ni katika harakati zake za kupunguza matumizi ya timu.

Man United tayari imepunguza wafanyakazi 450 tangu Ratcliffe aliponunua hisa ikiwamo na kuvunja mkataba wa kocha wa zamani wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson, aliyekuwa balozi wa klabu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily  Mail, wafanyakazi wengine 200 wa timu hiyo wako hatarini kupoteza ajira, wakiwamo baadhi walioitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu.

Inasemekana mmoja wa viongozi wa wafanyakazi ameambiwa kuwa nafasi yake iko hatarini licha ya kupandishwa cheo hivi karibuni.

Wakati huo huo, mfanyakazi mwingine wa muda mrefu pia ameambiwa yuko hatarini kuondolewa. Inaripotiwa kuwa mtu huyo anaheshimika sana katika tasnia ya soka, na kwamba mchango wake kwa timu ni mkubwa kutokana na uzoefu alionao.

Idara ya kusaka vipaji (scouting) ya klabu hiyo pia imeathirika kwa kiasi kikubwa, ambapo mkurugenzi wake, Steve Brown, ameondoka Old Trafford baada ya miaka tisa.

Inaripotiwa kuwa baadhi ya wafanyakazi wana hofu kwamba Ratcliffe "yuko hatarini kuondoa watu waliokuwa katika timu hiyo kwa muda mrefu na kufanya kazi kama mhimili wa timu".

Nyota wa zamani wa United, Eric Cantona, alimkosoa hadharani Ratcliffe kwa kitendo chake cha kufukuza wafanyakazi akisema: "Tangu Ratcliffe alipoingia, ni kama anajaribu kubomoa kila kitu na haeshimu mtu yeyote."

Aliongeza: "Ni muhimu kuwaheshimu watu hawa kama unavyomheshimu kocha wako na wachezaji. Tangu Ratcliffe afike, hali imekuwa tofauti kabisa. Hamtaki hata Sir Alex Ferguson mtu ambaye ni gwiji wa timu."

Hata hivyo, Ratcliffe ametetea hatua zake za kupunguza gharama, akidai kuwa klabu ingeishiwa fedha kufikia mwisho wa mwaka huu kama asingefanya hivyo.

Akizungumza na BBC, alisema: "Manchester United ingekuwa imeishiwa fedha kufikia mwisho wa mwaka huu wa 2025 licha ya mimi kuweka Dola 300 milioni na hata tusingesajili wachezaji. Tuko katika mchakato wa mabadiliko katika taasisi ambao haina utulivu."