Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi asema hii ya Wirtz ni aibu

BOSI Pict

Muktasari:

  • Liverpool imekubali kulipa Pauni 116 milioni kunasa saini ya kiungo huyo mshambuliaji, ambaye muda wowote wiki hii atakwenda Uingereza kukamilisha vipimo vya afya.

MUNICH, UJERUMANI: BOSI kubwa wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amekosoa uhamisho wa kiungo Florian Wirtz kuondoka Bayer Leverkusen kwenda kujiunga na Liverpool kuwa ni aibu kubwa Bundesliga kwa kupoteza mchezaji wa kiwango bora.

Liverpool imekubali kulipa Pauni 116 milioni kunasa saini ya kiungo huyo mshambuliaji, ambaye muda wowote wiki hii atakwenda Uingereza kukamilisha vipimo vya afya.

Kwenye dili hilo, Liverpool italipa Pauni 100 milioni kwanza kisha itaongeza Pauni 16 milioni baadaye, dili ambalo litaweka rekodi mpya kwenye uhamisho Uingereza. Manchester City na Bayern Munich nazo zilikuwa zinahitaji huduma ya mkali huyo mwenye umri wa miaka 22. Man City ilimtazama Wirtz kama mrithi wa Kevin De Bruyne, lakini ilijitoa kwenye mbio kutokana na kuona pesa nyingi na hivyo ikaamua kutumia Pauni 46.3 milioni kumsajili Tijjani Reijnders na Pauni 34 milioni kumchukua Rayan Cherki.

Bayern, ilishindwa kwenye vita hiyo na Wirtz alishawishika kujiunga na Liverpool kitu ambacho kimemwibua bosi wa Borussia Dortmund, Watzke akisema ni aibu kwani mchezaji huyo alipaswa kubaki Bundesliga na alidhani Bayern ingefanikisha dili la kumbazkiza.

“Hii ni aibu, hasa kwenye ligi ya Ujerumani DFL, mchezaji wa aina ya Florian Wirtz anaondoka kwenye Bundesliga,” alisema.

“Nisingekuwa na tatizo kama angekwenda FC Bayern. Ingekuwa vizuri sana kwenye Bundesliga. Angeenda kucheza vizuri na Musiala pale Munich, kwa sababu hao ni wachezaji wawili bora wangesaidiana.” Staa wa Bayern, Joshua Kimmich alizungumzia klabu yake kushindwa kwenye dili la Wirtz, alisema timu hiyo itakuwa na uhaba wa washambuliaji sababu Leroy Sane anakwenda Galatasaray na Thomas Muller ataondoka.