Benjamin Sesko ruhsa kuondoka RB Leipzig

Muktasari:

  • Sesko ambaye mkataba wake na Leipzig unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu uliomalizika alicheza mechi 41 za michuano yote na kufunga mabao 18, pia ametoa asisti mbili.

MSHAMBULIAJI wa RB Leipzig na Slovenia, Benjamin Sesko, 21, ana kipengele kwenye mkataba wake ambacho kinamruhusu kuondoka kwa Euro 65 milioni kabla ya mwezi huu kumalizika.

Sesko ambaye mkataba wake na Leipzig unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu uliomalizika alicheza mechi 41 za michuano yote na kufunga mabao 18, pia ametoa asisti mbili.


PARIS St-Germain imeiomba Napoli ikubali kupunguza bei ya mshambuliaji wao Khvicha Kvaratskhelia ambapo inahitaji Euro 100 milioni ili kumuuza wakati PSG wakiwa tayari kutoa Euro 60 milioni pekee.

Napoli kwa sasa inapambana ili kumpa mkataba mpya Khvicha ambao utakuwa na kipengele cha kumruhusu kwa bei maalum. Mkataba wa staa huyu unamalizika mwaka 2027.


MANCHESTER United imemweka kwenye rada mshambuliaji wa Wolves, Matheus Cunha, 25, na winga wa West Ham na Ghana, Mohammed Kudus, 23, ambao inahitaji kuwasajili katika dirisha hili.

Benchi la ufundi la Man United limependekeza majina haya kutokana na viwango bora walivyoonyesha kwa msimu uliomalizika. Mkataba wa Kudus unamalizika mwaka 2027.


NEWCASTLE United na Liverpool zote zinapambana kuiwania saini ya mshambuliaji wa Brentford na Cameroon, Bryan Mbeumo, 24, katika dirisha hili.

Timu hizi zinataka kumsajili Mbeumo baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu uliomalizika ambapo alicheza mechi 27 za michuano yote na kufunga mabao tisa.


MONACO inajiandaa kumuuza kiungo wao raia wa Ufaransa, Youssouf Fofana katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo Arsenal na Manchester United zote zimeonyesha nia ya kumsajili. Mabosi wa Monaco wanadaiwa kuhitaji kiasi kisichopungua Pauni 20 milioni ili kumuuza staa huyu mwenye umri wa miaka 25.


ARSENAL imeulizia uwezekano wa kuipata saini ya beki wa Barcelona na Senegal, Mikayil Faye, 19, katika dirisha hili baada ya kuvutiuwa na kiwango alichoonyesha msimu uliomalizika ambapo alicheza mechi 33 za michuano yote.

Mkataba wa Mikayil unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, Arsenal imeonyesha nia ya kumsajili baada ya kiwango bora alichoonyesha akiwa na timu za vijana za Barca.


KOCHA mpya wa Barcelona, Hansi Flick amependekeza jina la winga wa Atletico Madrid, Joao Felix, 24, asajiliwe katika dirisha hili aidha kwa mkopo au mazima.

Licha ya staa huyu wa kimataifa wa Ureno kutoonyesha kiwango kilichotarajiwa kwa msimu uliopita, Flick anaamini atafaa kwenye mfumo wake. Mkataba wake unamalizika mwaka 2029.