Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bei ya Rodrygo yawekwa ubaoni

RODRIGO Pict

Muktasari:

  • Arsenal inahitaji huduma ya winga huyo wa kushoto kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, ikilipa kipaumbele jina la Rodrygo na Nico Williams, ambaye anawindwa pia na Barcelona.

MADRID, HISPANIA: REAL Madrid imeripotiwa kuweka ubaoni bei anayouzwa staa wao, Rodrygo anayesakwa na Arsenal kuwa ni Euro 90 milioni.

Arsenal inahitaji huduma ya winga huyo wa kushoto kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, ikilipa kipaumbele jina la Rodrygo na Nico Williams, ambaye anawindwa pia na Barcelona.

Beki wa Arsenal, Gabriel alizungumza juu ya uvumi huo wa kuhusu Rodrygo, ambaye alimwelezea kuwa ni staa wa aina yake na kukiri winga huyo atakwenda kuungana naye Emirates.

“Ningepenga iwe hivyo bila shaka,” alisema Gabriel akimzungumzia Rodrygo.

“Ni wa aina yake. Nilishawaambia watu, ni mchezaji wa aina yake. Kama ingekuwa uamuzi wangu, ni wazi ningemtaka aje Arsenal!”

Kwa mujibu wa gazeti la Hispania la Cadena SER, kuna uwezekano mkubwa wa Rodrygo kwenda kujiunga na Arsenal. Staa huyo wa kimataifa wa Brazil ana mkataba wa miaka mitatu huko Los Blancos, wakati miamba hiyo ya Real Madrid imeshaweka wazi bei yake, kuwa Euro 90 milioni.

Hata hivyo, Arsenal si timu pekee inayohitaji saini ya Rodrygo, ambapo Manchester City, Chelsea na Tottenham nazo zilkijaribu kumnasa kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi la mwaka jana.

Rodrygo kwa sasa yupo na kikosi chake cha Real Madrid kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani na anatarajia kujadiliana na kocha mpya Xabi Alonso, ambaye alisema: “Ni mchezaji wa Madrid na nitafanya mazungumzo na kila mtu kwa sababu kuna ulazima wa kufanya hivyo.”

Ili kupata pesa za kukamilisha dili hilo, Arsenal itafungulia mlango wa kutokea mastaa wake kadhaa akiwamo Kieran Tierney, Jorginho, Nuno Tavares, Marquinhos, Oleksandr Zinchenko na Jakub Kiwior. huku ikipanga pia kumuuza mmoja kati ya Gabriel Martinelli au Leandro Trossard.