Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beckham amtetea Carrick kupewa ukocha wa kudumu Man United

Muktasari:

  • Beckham ameeleza sababu saba zinazomfanya aone kocha huyo wa muda anafaa kupewa nafasi hiyo kubwa baada ya kuibuka kwa ripoti kwamba Mashetani hao Wekundu wanahitaji kutafuta kocha mpya.

MANCHESTER, ENGLAND: GWIJI wa Manchester United, David Beckham, anaamini kocha Michael Carrick anastahili kupewa mkataba wa muda mrefu zaidi kwa sababu ya mambo saba.

Beckham ameeleza sababu saba zinazomfanya aone kocha huyo wa muda anafaa kupewa nafasi hiyo kubwa baada ya kuibuka kwa ripoti kwamba Mashetani hao Wekundu wanahitaji kutafuta kocha mpya.

Sababu ya kwanza, Beckham alitaja kuwa ni uzoefu wa Carrick. Kocha huyo alifanya kazi kwa misimu mitatu akifundisha Middlesbrough kabla ya kuchukua mikoba ya Man United kwa muda baada ya kufutwa kazi kwa Ruben Amorim.

Pia aliwahi kuwa kocha wa muda wa Man United mwaka 2021, ambapo alisimamia mechi tatu na akashinda dhidi ya Villarreal na Arsenal, na kutoa sare na Chelsea.

Sababu nyingine ni utulivu aliouleta ndani ya kikosi. Beckham anaamini Carrick ameleta hali ya nidhamu na utulivu unaohitajika ndani ya timu, akidai kuwa alinufaika kwa kufanya kazi chini ya kocha Sir Alex Ferguson kwa miaka saba alipokuwa mchezaji, jambo ambalo limemjenga kiuongozi.

Beckham pia anasema Carrick ana uweledi, utulivu na tabia njema, akifafanua kwamba: “Kuna namna ya utulivu na heshima katika mienendo yake, iwe anaposhangilia ushindi au hata anapokasirika. Hayo yote ni muhimu kwa kocha.”

Mwisho, Beckham alisifu uwezo wa Carrick wa kuiunganisha timu: “Namna alivyoiunganisha timu imekuwa ya ajabu sana. Kama mashabiki wa Man United, hiki ndicho tulichokuwa tunahitaji.”

Kwa sasa, umoja ndani ya timu unaonekana kuwa mkubwa, huku Carrick akishinda mechi saba kati ya kumi za mwanzo alizosimamia kama kocha mkuu.

Kocha huyo ameiongoza timu hiyo kupata ushindi muhimu dhidi ya wapinzani wao Manchester City, vinara wa ligi Arsenal, na wapinzani wa nafasi za juu Aston Villa.

Carrick ameifikisha Man United hadi nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England, ikiwa na tofauti ya pointi sita mbele ya bingwa mtetezi, Liverpool iliyo nafasi ya tano.

Kwa sasa inaonekana wazi kuwa Man United ipo katika nafasi nzuri ya kurejea Ligi ya Mabingwa Ulaya, mashindano ambayo mara ya mwisho kushiriki ilikuwa 2023 chini ya Erik ten Hag ambapo ilimaliza mkiani mwa kundi.

Kwa mujibu wa Oddschecker, Carrick ana nafasi kubwa ya kuwa kocha wa kudumu wa Manchester United kwa sasa, licha ya kuwepo kwa makocha wengine wanaohusishwa.