Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca ikimtosa Rashford fresh tu

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England yuko katikati ya mkopo wa msimu mzima katika klabu hiyo ya Catalan akitokea Manchester United na ameleta mchango mkubwa tangu kuwasili kwake.

BARCELONA, HISPANIA: NDO hivyo. Barcelona haitatozwa faini yoyote ya kifedha iwapo itaamua kusitisha mpango wa kumsajili jumla mshambuliaji Marcus Rashford mwishoni mwa msimu huu wakati mkopo wake utakapofika tamati.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England yuko katikati ya mkopo wa msimu mzima katika klabu hiyo ya Catalan akitokea Manchester United na ameleta mchango mkubwa tangu kuwasili kwake.

Amefunga mabao 10 na kutoa asisti 13 katika mashindano yote, huku Barca ikiongoza La Liga kwa tofauti ya pointi moja mbele ya Real Madrid. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 tayari ameonyesha nia ya kubaki Nou Camp kwa mkataba wa kudumu na kurejea Old Trafford msimu huu wa joto kunaonekana kuwa jambo lisilowezekana.

Klabu hiyo ya Hispania ina chaguo la Pauni 26 milioni kumsajili moja kwa moja kama mkurugenzi wa michezo Deco alivyoeleza masharti ya makubaliano yake ya muda. Akizungumza na SPORT, kiungo huyo wa zamani wa Chelsea FC na timu ya taifa ya Ureno aliulizwa kama Barcelona italipa adhabu iwapo haitamsajili Rashford moja kwa moja.

Alisema: “Hapana, ni mkopo tu na tuna chaguo.” Alipoulizwa kama wana nia ya kumbakisha kwa muda mrefu, Deco alijibu: “Ndiyo, bila shaka. Sidhani kama ilikuwa rahisi kuja hapa. Amecheza katika kiwango cha juu sana, akiwa chini ya presha kubwa katika klabu kama Manchester United.

“Kisha alitumia miezi sita Aston Villa, ambapo alifanya kazi nzuri sana. Kwa kweli, Aston Villa wangependa kumbakisha kama ingewezekana. Najua hili kwa sababu nimezungumza na watu wa huko. Lakini, alitaka kuja Barca pekee, na hilo ni jambo chanya sana.”

Deco alimpongeza Rashford kwa kukubali kupunguza mshahara wake ulioripotiwa kuwa Pauni 325,000 kwa wiki ili kufanikisha uhamisho wake kwenda Barcelona. Alisema: “Tuliweza kupata mkopo. Ukweli kwamba alipunguza mshahara wake ili hili lifanyike ni ishara tosha kwamba alitamani sana kuja hapa na tunafurahia hilo. Ni mchezaji anayechangia mengi kwa timu.”