Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atletico yaiaibisha Spurs ikipoteza mechi ya sita mfululizo

Muktasari:

  • Kinsky, aliyekuwa akicheza badala ya Guglielmo Vicario, alijikuta akianguka mara mbili na kusababisha mabao kwa Marcos Llorente na Julian Alvarez. Baada ya makosa hayo, kocha wa muda wa Spurs, Igor Tudor aliamua kumtoa mapema.

MSIMU mbaya wa Tottenham Hotspur umezidi kudhihirika zaidi baada ya kipa, Antonin Kinsky kutolewa uwanjani mapema katika dakika ya 17 wakati timu hiyo ikipokea kipigo cha aibu dhidi ya Atletico Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, usiku wa Machi 10, 2026.

Kinsky, aliyekuwa akicheza badala ya Guglielmo Vicario, alijikuta akianguka mara mbili na kusababisha mabao kwa Marcos Llorente na Julian Alvarez. Baada ya makosa hayo, kocha wa muda wa Spurs, Igor Tudor aliamua kumtoa mapema.

Katikati ya mkasa huo, beki Micky van de Ven pia aliteleza na kumpa nafasi Antoine Griezmann kufunga bao, kabla ya Robin Le Normand kuongeza la nne ndani ya dakika 23 za mwanzo katika moja ya mwanzo wa mechi za kushangaza zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa.

Bao la Pedro Porro lilipunguza maumivu kwa Spurs kwa muda mfupi tu, kabla ya Alvarez kufunga bao lake la pili dakika 10 baada ya mapumziko kufuatia shambulizi la kushtukiza lililoanza baada ya kipa Jan Oblak kuokoa kwa ustadi shuti la Richarlison.

Sasa Tudor anakabiliwa na maswali zaidi kuhusu mustakabali wake baada ya kupokea kipigo cha nne mfululizo, huku akishindwa kuizuia Spurs kuzama katika mgogoro mkubwa wa matokeo. Jumla Spurs imepoteza mechi sita mfululizo za mashindano yote inayoshiriki.

Ndoto za Kinsky kujihakikishia nafasi mbele ya Vicario zilivunjika mapema dakika ya sita alipoteleza na kuutoa mpira moja kwa moja kwa Ademola Lookman, ambaye alimpa pasi Llorente kufunga kwa utulivu.

Huo ulikuwa mwanzo wa kipindi cha mechi kilichokuwa cha kushangaza na cha kuaibisha Spurs msimu huu mbaya kwao.

Baadaye Van de Ven naye aliteleza na kumpa Griezmann nafasi ya kufunga bao la pili. Dakika chache baadaye Kinsky alianguka tena wakati akijaribu kupiga mpira wa kuokoa, jambo lililomruhusu Alvarez kuusukuma mpira wavuni kwa urahisi.

Tudor aliona imetosha na akaamua kumtoa Kinsky, akimwingiza Vicario. Kipa huyo wa Czech mwenye umri wa miaka 22 alifarijiwa na wachezaji wenzake na hata mashabiki wa Atletico walimpa makofi ya pole.

Mateso ya Spurs hayakuishia hapo, kwani Le Normand alifunga bao la nne baada ya vurugu eneo la hatari, kabla ya Porro kupunguza pengo kwa shuti la chini.

Hata hivyo, kipa wa Atletico Jan Oblak pia alifanya kosa lake alipotoa mpira vibaya na kumpa Dominic Solanke nafasi ya kufunga bao lingine kwa Spurs.

Usiku huo ulihitimishwa na tukio la kutisha zaidi kwa Spurs baada ya kugongana kwa vichwa kati ya Joao Palhinha na Cristian Romero. Palhinha alilazimika kutolewa nje, huku Romero akionekana bado kuathirika wakati timu hiyo ilimaliza mechi ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja.

Sasa Spurs itaikaribisha Atletico nyumbani kwenye Dimba la Tottenham katika mechi ya marudiano itakayochezwa Machi 18, 2026, ikiwa na deni la mabao 3-0 baada ya ugenini kuchapwa 5-2, pale Riyadh Air Metropolitano.