Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta: Ili kufuzu fainali UEFA tunahitaji kitu spesho Paris

Muktasari:

  • Goli la mapema la Ousmane Dembele lililodumu hadi mwisho, limewaacha Arsenal katika uhitaji wa kushinda kwa tofauti ya angalau bao moja dhidi ya Paris Saint-Germain katika mechi ya marudiano itakayochezwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa Parc des Princes.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema kikosi chake kitahitaji "kufanya jambo la kipekee jijini Paris" iwapo wanataka kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya nusu fainali katika dimba la Emirates, huku beki wake William Saliba akisema waliteseka sana katika mechi hiyo.

Goli la mapema la Ousmane Dembele lililodumu hadi mwisho, limewaacha Arsenal katika uhitaji wa kushinda kwa tofauti ya angalau bao moja dhidi ya Paris Saint-Germain katika mechi ya marudiano itakayochezwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa Parc des Princes.

"Kama unataka kushinda fainali ya Ligi ya Mabingwa, lazima ufanye jambo la kipekee. Tutahitaji kufanya jambo hilo la kipekee huko Paris ili tufike fainali," alisema Arteta ambaye timu yake ilipiga mashuti matano langoni katika mchezo wa mkondo wa kwanza.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Arsenal kushindwa kufunga bao katika mechi ya nyumbani ya Ligi ya Mabingwa tangu Februari 2016.

"Tuna nafasi kubwa ya kufika fainali hiyo. Kama nilivyosema, unahitaji kufanya jambo la kipekee katika mashindano haya ili kucheza fainali. Na muda wa kufanya hivyo upo huko Paris," aliongeza Arteta.

Arsenal hawajafika fainali ya Ligi ya Mabingwa tangu msimu wa 2005-06, wakati PSG wao wanapambana kutafuta taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa.

Msimu huu, PSG imezitoa timu mbili za England katika hatua za mtoano za michuano hii ikifanya hivyo kwa Liverpool na Aston Villa.

Saliba alisema wao kama wachezaji waliteseka sana katika dakika 20 za kwanza kwa sababu PSG waliumeza mchezo lakini bado wana matumaini ya kwenda katika hatua inayofuata.

"Bado haijaisha. Tunatumai kwamba tutashinda kule, hatuwezi kukata tamaa. Hii ni Ligi ya Mabingwa. Mambo mengi yanaweza kutokea."