Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta hataki kumtema Partey

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 31 amekuwa mmoja wa wachezaji bora kabisa kwenye timu hiyo msimu huu, lakini mkataba wake utafika ukomo mwezi ujao na kufanya hatima ya maisha yake kuwa kwenye mashaka makubwa.

LONDON, ENGLAND: KOCHA Mikel Arteta ameripotiwa kwamba kwa mara ya kwanza anataka kiungo Thomas Partey asainishwe mkataba mpya wa kuendelea kubaki Arsenal.

Kiungo huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 31 amekuwa mmoja wa wachezaji bora kabisa kwenye timu hiyo msimu huu, lakini mkataba wake utafika ukomo mwezi ujao na kufanya hatima ya maisha yake kuwa kwenye mashaka makubwa.

Klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid imeripotiwa kuwa miongoni mwa timu zinazofukuzia huduma ya kiungo huyo pamoja na klabu za Saudi Arabia.

Lakini, Arteta alishasema kwamba Arsenal ipo tayari kumpa Partey dili, ambaye amecheza mechi 50 msimu huu ofa ya mkataba mpya ili aendelee kubaki kwenye kikosi hicho cha Emirates.

Lakini, alipoulizwa kama Partey anabaki, Arteta alisema: “Ndio. Kuna maswali kidogo kwenye hilo, hivyo ngoja tuone. Thomas amekuwa na msimu bora. Kwa namna anavyocheza amekuwa matata kabisa. Ni mchezaji muhimu kwa timu yetu.”€

Wachezaji Kieran Tierney na Jorginho nao mikataba yao itafika tamati mwishoni mwa msimu huu, hivyo wawili hao watachezea Arsenal kwa mara ya mwisho itakapokipiga na Southampton, Jumapili.

Arsenal itakwenda kukipiga na timu hiyo kumaliza msimu wa Ligi Kuu England huku ikiwa haina presha yoyote kutokana na kuweka kibindoni tayari tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza ligi kwenye nafasi ya pili kwa misimu mitatu mfululizo.

Mabeki wa Arsenal, William Saliba na Jurrien Timber hawatakuwapo kwenye mechi hiyo ya mwisho wa msimu ya Arsenal kutokana na kusumbuliwa na maumivu.