Arteta abeba tuzo EPL

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amebeba tuzo ya kocha bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu England.
Tuzo hiyo  inakuwa ya tatu kwake msimu huu, tuzo ya kwanza alibeba mwezi Agosti mwaka jana pamoja na Novemba.

Arteta amebaba tuzo hiyo baada ya Arsenal kukukusanya pointi saba kwenye mechi za Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle, Tottenham na Manchester United.

Arsenal ilitoka suluhu dhidi ya Newcastle, kabla ya kumenyana na Tottenham na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, baadaye ikilipiza kisasi kwa kuifunga Man United mabao 3-2 uwanja wa Emirates.

Ikumbukwe mechi yao ya kwanza iliyochezwa Old Trafford, Man United iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. Mabao hayo yaliwekwa kimiani na Antony, Marcus Rashford akicheka na nyavu mara mbili.

Arteta anakuwa kocha wa kwanza Arsenal kubeba tuzo ya kocha bora kwa mara  tatu kwenye msimu mmoja katika historia ya klabu hiyo.

Arsenal imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City