Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yapasua kichwa kwa Sesko

SESKO Pict

Muktasari:

  • Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anahitaji mshambuliaji namba tisa na Mkurugenzi wa michezo, Andrea Berta analifanyia kazi hilo kwa sasa akiwa kwenye mazungumzo na wawakilishi wa Sesko pamoja na straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL inazidi kukatishwa tamaa na straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko juu ya madai yake ya mshahara anaohitaji ili kujiunga nao.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anahitaji mshambuliaji namba tisa na Mkurugenzi wa michezo, Andrea Berta analifanyia kazi hilo kwa sasa akiwa kwenye mazungumzo na wawakilishi wa Sesko pamoja na straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres.

Hata hivyo, kwa upande wa Gyokeres mambo yanaonekana kuwa magumu kutokana na ushindani mkubwa kutoka timu nyingine, pia hadi sasa ada yake ya uhamisho haijajulikana baada ya kuingia katika sintofahamu na timu yake.

Kutokana na hilo, Arsenal na Arteta wameelekezea nguvu kwa Sesko mwenye umri wa miaka 22, anayeichezea timu ya taifa ya Slovenia, wakitaka kumsajili na wako tayari kulipa Pauni 70 milioni kama ada ya uhamisho.

Lakini vyanzo vya ndani vinasema kambi ya Sesko inataka mkataba wa mshahara mkubwa kuliko kile ambacho timu imepanga kutoa na hilo linaweza kusababisha ugumu wa dili hilo.

Arsenal pia inakumbana na wakati mgumu katika kumsajili beki wa kati wa Crystal Palace na England, Guehi ambaye inadaiwa kuichagua Liverpool badala ya wao.

Inaelezwa Guehi alitaka uhakika wa kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza kutoka kwa kocha.

Hata hivyo, William Saliba na Gabriel Magalhaes kwa asilimia kubwa ndio wanaonekana kuwa chaguo la Arteta katika nafasi ya beki wa kati.

Kwa kuwa Liverpool inamuuza Jarell Quansah kwenda Bayer Leverkusen, majogoo hao wanataka kumsajili Guehi kama mbadala wake.

Beki huyo hataki kukaa benchi kwa sababu anataka kuwepo katika michuano ijayo ya Kombe la Dunia inayofanyika mwakani.