Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yaambiwa beba kipa Garcia ana kitu

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Garcia, 24, amekuwa kwenye rada za Arsenal kwa muda mrefu ambaye mara ya kwanza saini yake ilisakwa sana kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

BARCELONA, HISPANIA: KIPA wa zamani wa Arsenal, Wojciech Szczesny amebonyeza kitufe cha bluu juu ya mpango wa klabu yake hiyo kumtaka kumsajili kipa wa Espanyol, Joan Garcia akiiambia ana kitu.

Szczesny aliiambia Arsenal kwamba Garcia ni kipa bora kwenye La Liga.

Garcia, 24, amekuwa kwenye rada za Arsenal kwa muda mrefu ambaye mara ya kwanza saini yake ilisakwa sana kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Na sasa imeamua kuanzisha upya mpango wa kumsajili kipa huyo ili kwenda kushindania namba na David Raya katika msimu wa 2025-26.

Espanyol inafahamu pia kipa huyo ataondoka kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi, huku kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachobainisha bei anayouzwa kuwa ni Pauni 25 milioni. Na Szczesny ambaye kwa sasa anaitumikia Barcelona ameunga mkono mpango wa Garcia kuwindwa na Arsenal kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.

Szczesney alisema: “Nataka kumpongeza Joan Garcia; nadhani ni mmoja wa makipa bora La Liga na mustakabali bora kabisa mbele. Ni mmoja wa makipa bora Hispania na Ulaya.”

Kwa kauli hiyo ya Szczesney ina maana bosi mpya wa usajili wa Arsenal, Andrea Berta kuanza kupiga hesabu za kwenda kumchukua kipa huyo ili kuja kumpa changamoto Raya. Kiungo Martin Zubimendi ni mchezaji mwingine wa kutoka kwenye La Liga anayewindwa na Arsenal. Lakini, Szczesny amepitisha usajili wa Garcia kwenda kukipiga Emirates.