Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal wasiwasi wakiogopa historia

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Na tahadhari ya kuharibu hadithi mwisho wake si wa furaha. Manchester City watainua taji la Ligi Kuu England na mipango ya gwaride la basi kuzunguka Islington inaahirishwa tena kwa mwaka mwingine. Wasiwasi mkubwa umeanza kuwazonga.

LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa Arsenal waliondoka Emirates, Jumapili jioni wakiwa na hisia mbaya kwamba tayari wameshawahi kuona filamu hii.

Na tahadhari ya kuharibu hadithi mwisho wake si wa furaha. Manchester City watainua taji la Ligi Kuu England na mipango ya gwaride la basi kuzunguka Islington inaahirishwa tena kwa mwaka mwingine. Wasiwasi mkubwa umeanza kuwazonga.

Hofu kwa Arsenal kwa sasa ni historia inajirudia baada ya kipigo cha kushtukiza kutoka kwa Manchester United. Kikosi cha Mikel Arteta bado kinaongoza msimamo wa ligi kwa pointi nne mbele ya Man City na Aston Villa. Lakini pengo hilo lingekuwa kubwa zaidi kama Arsenal wasingeshindwa kushinda mechi zao tatu za mwisho za ligi.

ARS 01

Emirates ilikuwa imejaa wasiwasi Jumapili, kiasi usingewalaumu mashabiki wa Arsenal walioamua kukatisha furaha yao mapema. Kwa sasa ni mzunguko mbaya na presha kutoka jukwaani inaingia moja kwa moja uwanjani. Hata hivyo, Arteta na wachezaji wake pia wanapaswa kuwajibika kwa hali ya anga hiyo na ni rahisi kusema viwango vyao vya uchezaji vinachochea mvutano huo. Vyovyote vile, hali ikiendelea hivi, ni lazima ujiulize Emirates itakuwaje mwezi Aprili, ikizingatiwa tayari ni kama sufuria ya presha.

Man City wataikaribisha Arsenal mwezi huo katika mchezo ambao tayari unaonekana kuwa wa maamuzi makubwa zaidi kuliko ilivyodhaniwa siku kumi zilizopita.

Arsenal walikuwa maadui wao wakubwa wenyewe dhidi ya kikosi cha Man United kilichorejea katika kiwango kizuri. Kwa maneno ya mchambuzi wa Sky Sports, Gary Neville, yalikuwa maumivu waliyosababisha wao wenyewe. Baada ya kuchukua uongozi dakika ya 29, kikosi cha Arteta kilipoteza umakini na udhibiti wa mchezo.

ARS 02

Pasi mbaya ya Martin Zubimendi ilimpa Bryan Mbeumo nafasi ya kusawazisha, lakini ukweli ni bao hilo lilikuwa linakuja hata kabla ya kosa hilo. Katika dakika nane kati ya bao la kwanza na bao la Mbeumo, usahihi wa pasi wa Arsenal uliporomoka kwa asilimia 10 huku uzembe ukianza kuonekana.

Bao la United lilikuwa limeandikwa ukutani na ndivyo ilivyokuwa pia kwa kipigo hiki cha maumivu. Mechi mbili za ligi kabla ya hii zilikuwa sare tasa dhidi ya Liverpool na Nottingham Forest walioko chini ya msimamo. Matokeo hayo mabaya yalichochea wasiwasi.

Tofauti na Man City, Arsenal haina nafasi ya kumtegemea mfungaji kama Erling Haaland. Mabingwa watetezi, Liverpool ilikuwa ikimtegemea Mohamed Salah walipohitaji uchawi msimu uliopita.

ARS 03

Arsenal inakosa hilo. Mabao ya kujifunga ni mfungaji wao wa pili bora kwenye ligi msimu huu, wakiwa na mabao manne. Winga nyota Bukayo Saka kwa kawaida ndiye aliyekuwa anawaokoa, lakini sasa amecheza mechi 13 bila kufunga bao.

Kinachoongeza maumivu kwa Arsenal ni nje ya presha kali ya mbio za ubingwa, kikosi hiki huonekana tofauti kabisa. Usisahau, kipigo hiki dhidi ya kikosi cha Michael Carrick kilikuja baada ya ushindi mkubwa wa 3-1 dhidi ya Inter Milan, iliyocheza fainali za Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Arsenal ya Arteta pia ni miongoni mwa timu zenye mabao mengi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, ikiwa na mabao 20 baada ya kushinda mechi saba mfululizo. Ni miaka 22 tangu walipotwaa taji la Ligi Kuu England na tangu hapo wamekuwa wakikumbana na maumivu tu. Mashabiki wanakumbuka msimu wa 2007/08, wakati mambo yalipoanza kuyumba baada ya mshambuliaji Eduardo kuvunjika mguu kwenye mechi dhidi ya Birmingham. Kwa kikosi cha sasa, bado kina majeraha ya kumaliza nafasi ya pili kwa misimu mitatu mfululizo. Basi Arteta anatatua vipi tatizo hili?

Arteta na wachezaji wake wangefurahi sana mwanzoni mwa msimu huu kama wangeambiwa watakuwa wanaongoza ligi kwa pointi nne mwishoni mwa Januari.

Kipigo hiki dhidi ya Man United kinapaswa kuwa wakati wa Arsenal kujipanga upya, kujikusanya, na kujiandaa kisaikolojia kufukuza mizimu yote ya zamani. Wakifanya hivyo, wana ubora wa kutosha kutwaa taji lao la kwanza tangu enzi za Invincibles wa msimu wa 2003/04.