Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LEO NDO LEO! Emirates kitaumana Arsenal v Man United

Muktasari:

  • Mechi hiyo ya Ligi Kuu England inatambulika kwa kifupi kama Mikel Arteta dhidi ya Michael Carrick. Ar-senal itajaribu kuimarisha pengo lake la pointi kwenye kilele cha msimamo wa ligi, lakini Man United yenyewe itakwenda na lengo moja, kusimamisha mbio za ubingwa kwa The Gunners.

LONDON, ENGLAND: YANINI kuandikia mate. Wino si upo Emirates? Hizo ni tambo za mashabiki wa Arsenal na Manchester United wenye mazibizano yasiyokwisha.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu England inatambulika kwa kifupi kama Mikel Arteta dhidi ya Michael Carrick. Ar-senal itajaribu kuimarisha pengo lake la pointi kwenye kilele cha msimamo wa ligi, lakini Man United yenyewe itakwenda na lengo moja, kusimamisha mbio za ubingwa kwa The Gunners.

Shughuli ni leo Jumapili. Mashabiki wanatambiana, leo ni leo. Tofauti ya pointi 15 inazitenganisha timu hizi mbili kubwa kwenye msimamo wa ligi, lakini chini ya uongozi wa Carrick, hali nzuri tayari imerejea Old Trafford kwa Mashetani Wekundu.

Historia ya hivi karibuni ilijirudia kwa Arsenal katika mchezo wao wa mwisho wa ligi, ambapo vinara hao walishindwa kutumia ipasavyo nafasi waliyopewa ikizingatiwa kuwa ilitokana na ushindi wa Man United kwa Manchester City, ambao ni wapinzani wa karibu kwenye mbio za ubingwa.

Arsenal ilikuwa na fursa ya kuweka pengo la pointi kuleleni kufikia tisa, lakini kama ilivyokuwa raundi ya 21, kikosi cha Arteta kilishindwa kufunga katika sare ya 0-0 dhidi ya Nottingham Forest. Lakini, kushindwa kwa Man City na Aston Villa kunamaanisha kuwa Arsenal bado iko katika hali bora kuliko wiki iliyopita ikiwa kileleni kwa pointi saba kabla ya mechi ya washindani wao kwenye mbio za ubingwa, Man City haijamenyana na Wolves, jana Jumamosi.

Arsenal imetoka kukabiliana na Inter Milan, timu inayojulikana kwa uimara wa ulinzi, lakini chama la Arteta lilifanya kweli, likishinda 3-1 uwanjani San Siro, ushindi uliowahakikishia nafasi ya kuingia hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya huku ikiwa bado na mechi moja mkononi.

Sasa Arsenal inarejea nyumbani kaskazini mwa London, Emirates imekuwa ngome msimu huu kwa mi-amba hiyo ya kocha Arteta, ambao haijapoteza hata mechi moja kati ya 16 ilizocheza uwanjani hapo, ikishinda 14 na kuruhusu bao moja tu au pungufu katika kila mchezo.

Wakati Arsenal walishindwa kutumia udhaifu wa Man City, Man United ilifanya kazi yake ipasavyo, ikipuuza presha na machafuko ya nje ya uwanja ili kuwashangaza mahasimu wao wakubwa kwa ushin-di wa kiwango cha juu Old Trafford.

Carrick, aliyerejea upya kama kocha, alishuhudia Bryan Mbeumo na Patrick Dorgu wakifunga katika ushindi huo wa mabao 2-0, ushindi wa kwanza wa Man United katika mashindano yoyote tangu Ruben Amorim alipoiongoza timu kushinda 1-0 dhidi ya Newcastle United kwenye Boxing Day.

Ikirejea kwenye mbio za kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mashetani Wekundu wanaanza wikendi wakiwa pointi moja nyuma ya Liverpool iliyopo nafasi ya tano.

Kwa kweli, Man United imefunga bao katika mechi zao 11 za mwisho katika mashindano yote, pamoja na mechi tisa mfululizo za ugenini, ingawa wamekuwa pia wakiruhusu nyavu zao kuguswa katika mechi zote ilizocheza ugenini ndani ya kipindi hicho.

Man United imeruhusu bao katika kila mchezo wa ugenini wa msimu wa 2025–26, takwimu mbaya ka-bla ya kukutana na Arsenal ambayo imewafunga Man United mara tano katika michezo sita ya mwisho ya ligi, ikiwemo ushindi wa 1-0, Agosti mwaka jana uwanjani Old Trafford.

Habari njema kwa Arteta, kwani tatizo la majeruhi kwenye safu ya ulinzi linaanza kupungua. Riccardo Calafiori (misuli) na Piero Hincapie (paja) walirejea mazoezini Ijumaa, ingawa kocha hakuthibitisha ka-ma watakuwa tayari kwa mechi.

Hata hivyo, wawili hao wanaonekana kuwa katika hali nzuri ya kurejea Jumapili, huku Max Dowman akiwa mchezaji pekee wa Arsenal anayeendelea kuuguza jeraha la kifundo cha mguu. Mabao mawili ya Gabriel Jesus alipoanza dhidi ya Inter, pamoja na mchango mzuri wa Viktor Gyokeres alipotokea benchini, vimeleta kitendawili kigumu kwa Arteta katika upangaji wa kikosi chake katika safu ya ush-ambuliaji. Hata hivyo, Gyokeres ana nafasi kubwa ya kuanza.

Kwa upande wa Man United, Carrick bado atamkosa Matthijs de Ligt (jeraha la mgongo), huku Joshua Zirkzee akiwa shakani kutokana na maumivu madogo.

Mshindi wa pili wa AFCON 2025, Noussair Mazraoui anatarajiwa kurejea, lakini Carrick hatapenda ku-badilisha kikosi kilichoshinda dhidi ya Man City, jambo linalomaanisha Kobbie Mainoo kuanza tena kwenye kiungo wa kati. Mainoo atacheza sambamba na Casemiro, ambaye amethibitishwa kuondoka mwishoni mwa msimu, pamoja na Bruno Fernandes, aliyetengeneza nafasi sita za mashambulizi kwenye mechi dhidi ya Man City. Kazi ipo.

Vikosi Vinavyotarajiwa;

Arsenal: Raya; Timber, Saliba, Gabriel, Hincapie; Odegaard, Zubimendi, Rice; Saka, Gyökeres, Trossard

Man United: Lammens; Dalot, Maguire, Martinez, Shaw; Mainoo, Casemiro; Diallo, Fernandes, Dorgu; Mbeumo