Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal mpo? Msikieni ndugu yake Gyokeres

Muktasari:

  • Gyokeres, 26, ni moja ya mastraika wanaosakwa kwa nguvu zote huko Ulaya baada ya kufanya vizuri misimu miwili iliyopita, akifunga mabao 96 katika mechi 101 alizochezea klabu hiyo ya Ureno.

LISBON, URENO: MMOJA wa wanafamilia ya straika Viktor Gyokeres amedai anaamini staa ataendelea kubaki kwenye kikosi cha Sporting CP licha ya kuhusishwa kwenda Arsenal.

Gyokeres, 26, ni moja ya mastraika wanaosakwa kwa nguvu zote huko Ulaya baada ya kufanya vizuri misimu miwili iliyopita, akifunga mabao 96 katika mechi 101 alizochezea klabu hiyo ya Ureno.

Arsenal imekuwa ikimfukuzia mshambuliaji huyo wa Sweden ili kumaliza tatizo linaloikabili la kuwa na uhakika wa mabao.

Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta ameripotiwa kuvutiwa na Gyokeres akijaribu kumshawishi kocha Mikel Arteta kuamini ni mtu sahihi kwenye kuongoza safu ya ushambuliaji.

Gyokeres aliendeleza moto alipotikisa nyavu kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Vitoria wikiendi iliyopita kusaidia timu hiyo kubeba taji la pili mfululizo la Liga Portugal.

Akizungumza baada ya mechi mwanafamilia mmoja wa Gyokeres, anayefahamika kwa jina la Chris alibainisha kitu kinachomhusu straika huyo.

Akiwa amevaa skafu ya Sporting na jezi ya timu hiyo, Chris alisema: “Nimefurahi sana, hii ni safi. Tulikuwa hapa mwaka jana, tupo hapa tena na watu walewale. Hii ni kali, nashindwa kuelezea!”

Chris alikwenda mbali zaidi na kufichua kwamba familia imeshajadiliana juu ya mpango wa uhamisho wa Viktor, wakati alipoulizwa kama mchezaji huyo atabaki Sporting, alisema: “Ndio, bila shaka... jana wakati tunapata mlo wa usiku tulijadili na kuamua atabaki.” Na maelezo hayo aliyatoa kwenye maneno manne tu alipoulizwa kama Gyokeres atabaki kwenye klabu hiyo wakati wa dirisha la majira ya kiangazi aliposema: “Ndio, tunafikiri itakuwa hivyo.”

Haifahamiki kama bosi wa usajili wa Arsenal, Berta amesikiliza maelezo ya mwanafamilia huyo wa Gyokeres.