Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal majanga, Havertz nje msimu mzima

Muktasari:

  • Baada ya Gabriel Jesus kuumia misuli ya goti, Havertz alibaki kuwa chaguo pekee la Arsenal katika nafasi ya mshambuliaji wa kati.

DUBAI, UAE: STAA wa Arsenal, Kai Havertz atakosekana uwanjani kwa kipindi chote cha msimu kilichobaki baada ya kupata tatizo la maumivu ya misuli wakati akiwa mazoezi kwenye kambi ya timu hiyo, huko Dubai.

Baada ya Gabriel Jesus kuumia misuli ya goti, Havertz alibaki kuwa chaguo pekee la Arsenal katika nafasi ya mshambuliaji wa kati.

Kikosi hicho chenye maskani yake Emirates, kinachonolewa na kocha Mhispaniola, Mikel Arteta kilishindwa kufanya usajili wa straika kupitia dirisha la majira ya kiangazi, uamuzi ambao sasa utawaweka kwenye wakati mgumu baada ya kuumia Havertz.

Havertz alipatwa na maumivu ya misuli ya nyuma ya paja wakati wa mazoezi ya timu hiyo iliyoweka kambi Dubai, ili kujifua katika mazingira ya hali ya hewa ya joto. Kuumia kwa mchezaji huyo ni pigo kubwa kwa Arsenal kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arsenal kwa sasa ipo nyuma kwa pointi sita dhidi ya vinara Liverpool katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Kwa sasa bado haijafahamika kama Havertz, 25, atahitaji kufanyiwa upasuaji, lakini kinachofahamika ni kwamba anapaswa tu kujiweka fiti kwa ajili ya msimu wa 2025-26. Hilo ni pigo kubwa kwa Havertz, ambaye kwa msimu huu ametumikia karibu katika kila mechi, akifunga mabao 15 na asisti tano katika mechi 34 alizocheza kwenye michuano yote. Majeruhi hayo ya Havertz yamemwacha Arteta katika maswali mengi namna atakavyofanya kwenye mbio za ubingwa.

Na sasa atalazimika kumtumia mmoja wa wachezaji Leandro Trossard, Ethan Nwaneri na Raheem Sterling kwenye majukumu ya nafasi ya mshambuliaji wa kati. Lakini, Arteta anaweza pia kumtumia straika wa kikosi cha U-21, Nathan Butler-Oyedeji na winga wa kikosi hicho cha vijana, Ismeal Kabia kama machaguo mengine katika kuziba pengo hilo la mshambuliaji wa kati.

Arsenal iliripotiwa kuwa na mpango wa kusajili straika mpya kupitia dirisha la Januari baada ya Jesus kuumia kwenye mechi ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United. Katika kipindi hicho ilihusishwa na mshambuliaji wa Newcastle United, Alexander Isak, lakini baadaye aliachana na mpango huo.

Arteta alijaribu kwenda kumsajili straika wa Aston Villa, Ollie Watkins, lakini alishuhudia ofa yake ya Pauni 60 milioni ikigomewa na mabosi wa klabu hiyo yenye maskani yake Villa Park. Baada ya hapo, Arteta alidai kwamba anaamini Havertz atabeba majukumu ya kwenda kuificha timu hiyo kwenye malengo ya kunyakua ubingwa kabla ya Mjerumani huyo naye kuumia, ikiwa ni siku chache kabla ya kukabiliana na Leicester City katika Ligi Kuu England, Jumamosi.

Na sasa Arteta atalazimika kutafuta suluhisho la haraka la nani atacheza katika nafasi hiyo ya mshambuliaji wa kati kuanzia kwenye kipute dhidi ya Leicester City.