Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal ina mechi saba bila Saliba

SALIBA Pict

Muktasari:

  • Ripoti za kutoka Ufaransa zinafichua kwamba beki huyo Saliba atakuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua wiki tatu hadi nne. Beki huyo alitolewa uwanjani na kushindwa kumaliza mechi wakati Arsenal ikipokumbana na kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Liverpool kwenye Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: KOCHA, Mikel Arteta kijasho kinamtoka jinsi namna atakavyokipanga kikosi chake cha Arsenal kutokana na kumkosa beki wa kati, William Saliba kwenye mechi saba muhimu.

Ripoti za kutoka Ufaransa zinafichua kwamba beki huyo Saliba atakuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua wiki tatu hadi nne. Beki huyo alitolewa uwanjani na kushindwa kumaliza mechi wakati Arsenal ikipokumbana na kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Liverpool kwenye Ligi Kuu England.

Saliba alipata maumivu ya enka, ambayo pia yamemfanya ajiweke kando kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa, Les Bleus. Kutokana na hilo, Saliba, 24, atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja wakati Arsenal ikijiandaa kurudi kwenye makali yake wakati michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikirejea badaa ya mechi za kimataifa.

Mapema wiki hii, taarifa kutoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa, ilisomeka: "William Saliba, ambaye alianzishwa kwenye mechi dhidi ya Liverpool, Jumapili iliyopita, alilazimika kutoka dakika ya tano. Hakupata heshima ya kuitwa kwenye kambi ya timu ya taifa. Anasumbuliwa na maumivu ya enka. Baada ya majadiliano na Franck Le Gall, daktari wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps alithibitisha kutokuwapo William Saliba. Kocha wa timu ya taifa ameamua kumuita Benjamin Pavard."

Saliba atakosa mechi dhidi ya Nottingham Forest, Athletic Bilbao, Manchester City na ile ya Kombe la Ligi dhidi ya Port Vale. Kama staa huyo wa Arsenal atashindwa kupona kwa wakati atakosa pia mechi za Newcastle, Olympiacos na West Ham United.

Beki mpya aliyesajiliwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka huu kwa ada ya Pauni 13 milioni akitokea Valencia, Cristhian Mosquera, 21, ndiye aliyeingizwa kuchukua nafasi ya Saliba dhidi ya Liverpool.

Kocha Arteta alifanya uboreshaji mkubwa kwenye safu yake ya ulinzi kwenye dirisha lililopita wakati alipomchukua Piero Hincapie kutoka Bayer Leverkusen kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Hincapie, 23, aliyetua Emirates kwa mkopo na timu hiyo inaweza kumchukua jumla kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwakani.

Arteta alisema: "Tunashukuru Mungu tunaye Mosquera, mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Leeds na mwanzoni hatukumtegemea kumtumia Anfield na nadhani ni mzuri sana."