Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal imetema mzigo, Liverpool njia nyeupe

Muktasari:

  • Matumaini ya Arsenal kubeba taji la msimu huu yameyeyuka baada ya kuambulia pointi moja tu huko City Ground.

NOTTINGHAM, ENGLAND: ARSENAL imebanwa mbavu na Nottingham Forest kwa kutoka suluhu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England matokeo ambayo tafsiri yake nyepesi kwamba kikosi hicho cha Mikel Arteta kimekubali yaishe kwenye mbio za kusaka ubingwa msimu huu.

Matumaini ya Arsenal kubeba taji la msimu huu yameyeyuka baada ya kuambulia pointi moja tu huko City Ground.

Wakati huo Forest ikiendelea kubaki kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu England, lakini sasa ikiwa imecheza mechi tatu bila ya ushindi kitu kinachowapa presha katika harakati zao za kubaki Top Four.

Matokeo ya mchezo huo yamekuwa na athari kubwa sana kwenye mipango ya Arsenal ya msimu huu, na kwa sasa imeachwa nyuma kwa pointi 13 na vinara Liverpool.

Katika kuweka hai matumaini ya ubingwa, Arsenal ilihitaji kuifunga Forest, lakini ilishindwa kufanya hivyo na mbaya zaidi kwa kipindi chote cha kwanza haijapiga shuti lolote kulenga goli.

Baada ya kubanwa na Forest, dua zao zilikuwa kwa Liverpool ipoteze mbele ya Newcastle, lakini miamba hiyo ya Anfield ilishinda 2-0 na kufanya pengo la pointi kileleni kufikia 13.

Na Arsenal sasa imebakiza mechi 11 tu za kufanya maajabu ya kunyakua taji hilo, huku ikiomba Liverpool ipoteze mechi si chini ya tano kati ya 10 zilizobaki.

Silaha, ambayo Arsenal ilikuwa ikitamba nayo mwanzoni mwa msimu huu ya mipira ya kutenga kwa sasa imekuwa haina msaada tena kwa timu hiyo.

Kwenye mchezo huo wa Forest, Arsenal ilipiga kona na mipira ya adhabu mara nyingi, lakini hakuna wowote uliokuwa tishio kwa wapinzani.

Mwanzoni mwa msimu, mtaalamu wa mipira ya kitenga kwenye kikosi cha Arsenal, Nicolas Jover alipata sifa nyingi sana kutokana na mabao iliyokuwa ikifunga timu hiyo kupitia mipira ya kona na adhabu, lakini sasa hali ni ngumu, jambo linalomfanya Jover kulazimika kuboresha mazoezi yake upya.

Baada ya Arteta kushindwa kunasa straika kwenye dirisha lililopita na kisha kupoteza washambuliaji wake wote kwa majeruhi, kocha huyo amekuwa akimwamini Mhispaniola mwenzake, Mikel Merino kucheza kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati, lakini mambo yamekuwa tofauti, ambapo kwenye mechi ya Forest, Merino, 28, aligusa mpira mara nne tu ndani ya boksi la Forest.