Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arne Slot kupewa dili jipya Anfield

Muktasari:

  • Klopp alijiunga na Liverpool, Oktoba 2015, aliposaini mkataba wa miaka mitatu, lakini baada ya kumaliza msimu wa kwanza tu, alisaini dili jingine jipya la miaka sita.

LIVERPOOL, ENGLAND: MABOSI wa Liverpool wameripotiwa kuwa na mpango wa kumpa dili jipya kocha Arne Slot baada ya Mdachi huyo kufunguka kwamba anataka abaki kwenye timu hiyo muda mrefu kama Jurgen Klopp.

Klopp alijiunga na Liverpool, Oktoba 2015, aliposaini mkataba wa miaka mitatu, lakini baada ya kumaliza msimu wa kwanza tu, alisaini dili jingine jipya la miaka sita.

Na sasa wamiliki wa klabu hiyo ya Liverpool, Fenway Sports Group (FSG) anataka kumpa Slot dili kama hilo baada ya awali kusaini miaka mitatu, huku msimu wake wa kwanza akifanikiwa kushinda ubingwa Ligi Kuu England. Awali kocha Slot alificha kama tupo kwenye mazungumzo ya dili jipya, lakini sasa imefichuka kwamba mabosi wake wa huko Anfield wanataka abaki kwa muda mrefu zaidi.

Lakini, alipoulizwa kama ataamua kuiga alivyofanya mtangulizi wake Klopp kwa kukaa kwenye timu hiyo kwa miaka mingi, alisema: “Nitaangalia. Hii klabu ina historia ya kukaa na makocha wake kwa muda mrefu na tuliona pia kina Arsene Wenger na Sir Alex Ferguson.

“Nafikiria kwenye ujumla, kwenye soka na maisha, kunahitajika utulivu mkubwa. Pengine hapa England panaweza kuwa tofauti. Ikiwa hivyo, basi najiona nitakuwa hapa kwa muda mrefu kwa sababu hii ni klabu kubwa na nimekuwa na furaha kubwa kuwa hapa.”