Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ancelotti atajwa kutua Saudia

Muktasari:

  • Baada ya Real Madrid kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Arsenal mapema mwezi huu, ripoti zilianza kuenea kwamba Kati ya sehemu alizodaiwa kuwa anaweza kutua kocha huyo raia wa Italia ni Brazil kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo ya taifa kuelekea fainali za Kombe la Dunia la 2026 litakalofanyika Amerika ya Kaskazini.

MADRID, HISPANIA: KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti huenda akatimkia Saudi Arabia licha ya hivi karibuni kudaiwa kufikia makubaliano ya kuchukua mikoba ya kuifundisha timu ya taifa ya Brazil.

Baada ya Real Madrid kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Arsenal mapema mwezi huu, ripoti zilianza kuenea kwamba Kati ya sehemu alizodaiwa kuwa anaweza kutua kocha huyo raia wa Italia ni Brazil kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo ya taifa kuelekea fainali za Kombe la Dunia la 2026 litakalofanyika Amerika ya Kaskazini.

Hata hivyo, ripoti mpya zimeibua uwezekano wa ajira mpya isiyotarajiwa, na kuleta wasiwasi mkubwa kuhusu madai ya kwamba Ancelotti angechukua mikoba ya Brazil.

Ripoti za awali zilipendekeza kwamba Ancelotti angeondoka Real Madrid mara tu baada ya fainali ya Copa del Rey dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Barcelona ambayo walipoteza.

Kwa mujibu wa gazeti la Marca nchini Hispania, Ancelotti alibadili uamuzi wake katika dakika za mwisho kuhusu kujiunga na timu ya taifa ya Brazil baada ya kusafiri hadi London siku ya Jumatatu kwa ajili ya kusaini mkataba na mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia.

Ingawa awali alithibitisha kwamba angesaini mkataba siku ya Jumanne, sasa anaripotiwa kuwa ameamua kutoendeleza mpango huo, na tayari amemjulisha Rais wa Shirikisho la Soka la Brazil, Ednaldo Rodrigues, kuhusu uamuzi huo.

Badala yake, sasa inaaminika kwamba Ancelotti anaweza kubaki Real Madrid hadi michuano ya Kombe la Dunia kwa Klabu itakapomalizika na baadaye kutimkia Saudi Arabia.

Inadaiwa kocha huyu amepokea ofa nono kutoka kwa matajiri wa Saudia ambao wapo tayari kumlipa Euro 50 milioni kwa msimu, kiasi kitakachomfanya kuwa kocha aliyewahi kulipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya soka.

Wakati haya yakiendelea, beki kisiki wa Madrid, Antonio Rudiger amekumbana na adhabu ya kufungiwa kucheza mechi sita baada ya kitendo chake katika fainali ya Copa del Rey cha kumrushia mwamuzi barafu.