Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ataka wachezaji Man United wazomewe

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Mashetani Wekundu walifungwa 1-0 na ASEAN All-Stars huko Malaysia siku ya Jumatano, mechi ambayo ilizidi kuwa pigo kwa mashabiki wao ambao wamekuwa na huzuni muda mwingi wa msimu uliopita kutokana na matokeo ya ovyo.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amekiri kuwa wachezaji wake waliopo Manchester United huenda wanahitaji kuzomewa na mashabiki ili kuwafanya warudi katika mstari.

Mashetani Wekundu walifungwa 1-0 na ASEAN All-Stars huko Malaysia siku ya Jumatano, mechi ambayo ilizidi kuwa pigo kwa mashabiki wao ambao wamekuwa na huzuni muda mwingi wa msimu uliopita kutokana na matokeo ya ovyo.

Man United walipokea kichapo hicho mbele ya mashabiki takriban 70,000, siku tatu tu baada ya kufunga msimu wao wa kusikitisha wa Ligi Kuu kwa ushindi dhidi ya Aston Villa.

Baada ya kichapo hicho cha aibu, mashabiki wa Manchester United waliwazomea wachezaji wao.

Kuhusu kelele hizo za kuzomewa, kocha Amorim alikiri:

“Najihisi kila wakati kuwa na hatia kwa matokeo ya timu tangu nilipofika hapa katika mechi yangu ya kwanza. Zomea za mashabiki, labda ni kitu tunachohitaji kwa sababu kila mechi tuliyopoteza kwenye Ligi Kuu wao walikuwa pale. Tusubiri tuone msimu ujao.”

Akizungumza na MUTV, kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 alikiri kuwa timu yake “hujikwaa kila mara.”

Kocha huyo wa zamani wa Sporting CP alisema: “Ndiyo, ni matokeo ya kuvunja moyo, lakini hakuna majeruhi na uwanja ulikuwa mgumu. Tunapaswa kushinda mechi kama hizi, haijalishi ni mazingira gani. Tunapaswa kuwa na msukumo huo ndani yetu kwenye kila mechi.

“Jambo la muhimu ni kuwa hakuna majeruhi licha ya hali ya hewa, na kufika hapa kwa siku ya mechi. Si kisingizio, tulipaswa kucheza vizuri zaidi.”

Manchester United watarejea uwanjani tena Ijumaa hii ambapo watakutana na timu ya taifa ya  Hong Kong.