Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ahusishwa kibarua cha Mourinho

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Kocha mwingine Mreno Jose Mourinho yuko kwenye presha kubwa Benfica baada ya timu hiyo kuachwa nyuma kwa pointi 10 katika mbio za ubingwa wa ligi. Pia iko nafasi ya 25 kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LISBON, URENO: RUBEN Amorim ameripotiwa yupo kwenye hatua nzuri ya kupata kazi mpya huko kwao Ureno ikiwa ni siku chache tu tangu alipofutwa kazi Manchester United, Jumatatu iliyopita.

Kocha mwingine Mreno Jose Mourinho yuko kwenye presha kubwa Benfica baada ya timu hiyo kuachwa nyuma kwa pointi 10 katika mbio za ubingwa wa ligi. Pia iko nafasi ya 25 kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ripoti zinafichua kwamba Amorim yuko kwenye nafasi ya juu kabisa kuchukua kibarua hicho cha Mourinho, ambaye aliwahi pia kuinoa Man United.

Inadaiwa kuwa nafasi ya Mourinho inazidi kuwa hatarini, huku klabu hiyo ikiwa na historia ya kumfuatilia Amorim.

Amorim aliwahi kukataa uvumi wa kurejea Benfica mwezi Septemba baada ya mgombea wa urais wa klabu, Joao Noronha Lopes, kukiri kuwa angependa kumleta Amorim kikosini.

Lopes hata alihudhuria mechi Old Trafford baada ya kuweka wazi kuwa anamwona Amorim kama kocha wa baadaye wa Benfica, lakini hatimaye alishindwa katika uchaguzi dhidi ya gwiji wa klabu hiyo, Rui Costa.

Amorim alifukuzwa kazi Man United, Jumatatu iliyopita baada ya kutoa kauli kali kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Leeds United siku iliyotangulia.

Kocha huyo raia wa Ureno alisisitiza kuwa alitaka kuwa meneja kamili, siyo kocha mkuu pekee, na alionekana kuwakosoa mkurugenzi wa michezo Jason Wilcox pamoja na mkuu wa usajili Christopher Vivell.

Madhara yaliyotokea nyuma ya pazia hayakuweza kurekebishwa na Amorim alilazimika kuondoka Man United akiwa ndiye meneja mbaya zaidi katika historia ya klabu hiyo enzi ya Ligi Kuu England, akiwa na asilimia ya ushindi ya asilimia 31.9 pekee.

Hata hivyo, aliachana na klabu hiyo akiwa na fidia ya Pauni 12 milioni, jambo lililomfanya pia kuwa kocha ghali zaidi kuwahi kulipwa na Man United.

Mourinho alizungumzia kuondoka kwa Amorim mapema wiki hii, amesema: “Kilichotokea kwa Ruben ni jambo ambalo mwenyewe pekee anaweza kulichambua.”