Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tatizo la Amorim ni wachezaji saba

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Ndani ya uwanja kocha Amorim ameisimamia Man United katika mechi 47, ameshida 15, sare 13 na vichapo 19, huku akiwa na wastani wa ushindi wa asilimia 31.9. Namba hazidanganyi!

MANCHESTER, ENGLAND: MJADALA wa moto kwa sasa ni kuhusu kocha Ruben Amorim. Manchester United imemfuta kazi kocha huyo, lakini kinachojadiliwa, je uamuzi huo ni sahihi kufanyika kwa sasa au ameonewa na kwamba alistahili kupewa muda? Majibu ni mengi na kila upande una hoja zake.

Ndani ya uwanja kocha Amorim ameisimamia Man United katika mechi 47, ameshida 15, sare 13 na vichapo 19, huku akiwa na wastani wa ushindi wa asilimia 31.9. Namba hazidanganyi!

Katika kipindi chake Amorim, umekuwa na mambo mengi ikiwamo uongozi wa Man United kuripotiwa kuzuia usajili wa mastaa saba wakubwa ambao Mreno huyo alihitaji huduma zao Old Trafford.

Man United ilitumia Pauni 256 milioni kwenye usajili wa mastaa wapya kwa kipindi cha miezi 14 ambayo ilikuwa chini ya kocha huyo, lakini Mreno huyo hakuridhishwa na usajili uliofanywa na klabu hiyo.

PAZ 02

Amorim, 40, alifukuzwa kazi Man United baada ya kuikosoa hadharani bodi ya wakurugenzi kuhusu malengo yake kwenye usajili wa wachezaji.

Kinachoripotiwa ni kwamba tatizo kubwa la Amorim lilikuwa yeye kupendekeza malengo tofauti na orodha fupi iliyoundwa na Mkurugenzi wa Michezo, Jason Wilcox na Mkurugenzi wa Usajili, Christopher Vivell.

Kingine ni kwamba Amorim ametaka kufahamika kama “meneja” na sio “kocha mkuu” katika kauli yake ya kushtua baada ya Man United kutoka sare ya bao 1-1 na Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu England, Jumapili iliyopita.

Amorim alitaka kuwa na udhibiti zaidi katika uamuzi, hivyo alikasirishwa na mipango ya awali ya usajili, ambao kwa kiasi kikubwa ulisimamiwa na bosi Wilcox na wenzake.

PAZ 05

Baada ya makipa Andre Onana na Altay Bayindir kuonyesha kiwango kisichoridhisha, Amorim alitaka kipa aliyethibitishwa Ligi Kuu England na bingwa wa Kombe la Dunia, Muargentina, Emi Martinez, aje Man United kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Martinez, 33, alikuwa Villa Park akisubiri simu kutoka Man United katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili, lakini uhamisho huo ungeigharimu miamba hiyo ya Old Trafford kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni.

Lakini, uongozi wa Man United chini ya mmiliki mwenza, bilionea Sir Jim Ratcliffe uliona kiwango hicho cha pesa ni kikubwa na hivyo kwenda kunasa saini ya kipa kijana na asiyejulikana sana, Senne Lammens, 23. Kipa huyo alinaswa kwa Pauni 18.2 milioni na amekuwa kwenye kiwango bora kabisa huko Old Trafford.

PAZ 07

Taarifa zaidi zinadai, Amorim alitaka Man United ivamie hapohapo Aston Villa kumchukua straika Ollie Watkins, kabla klabu hiyo haijalipa Pauni 74 milioni kumsajili straika Benjamin Sesko.

Mkuu wa usajili, Vivell alizingatia zaidi ishu ya baadaye na ndiyo maana alipitisha usajili wa Sesko badala ya Watkins. Beki wa kushoto wa Paris Saint-Germain, Nuno Mendes, naye alikuwa chaguo la kwanza la kocha Amorim, akimtaka asajiliwe na Man United ili akakipige chini yake huko Old Trafford, lakini mabosi waliamua kwenda kumchukua Patrick Dorgu kutoka Lecce.

Hasira za Amorim pia zilihusisha kukataliwa kwa wachezaji kadhaa kutoka klabu yake ya zamani Sporting Lisbon, ambao alitaka wasajiliwe Man United. Wachezaji hao ni Geovany Quenda, Ousmane Diomande, Salvador Blopa na Morten Hjulmand.

Man United ilichukua tahadhari ya kukwepa kuingia kwenye njia ileile iliyomruhusu kocha wa zamani, Erik ten Hag kusajili wachezaji kadhaa kutoka kwenye timu aliyotoka, Ajax Amsterdam ya Uholanzi.

PAZ 01

Lakini, Man United ilikuwa tayari kumchukua Quenda, 18 na mazungumzo yalifika kwenye hatua nzuri kabisa ya makubaliano, lakini mchezaji huyo kubadili uamuzi na kujiunga na Chelsea kwa ada ya Pauni 42 milioni, ambapo atatua Stamford Bridge rasmi katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Quenda alijiunga na Sporting mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 13, huku Amorim akiwasili mwaka mmoja baadaye.

Taarifa za kutoka ndani Man United zinadai kwamba mpango wa kumsajili Quenda ulipungua nguvu kwa sababu ana wasifu unaofanana na Amad Diallo.

Hjulmand alikuwa mchezaji ambaye Amorim aliamini angeweza kutatua matatizo kwenye safu ya kiungo ya kati na ambaye pia asingehitaji kufundishwa mfumo wa mbinu wa timu kutoka kwenye staili yake ya uchezaji ya 3-4-2-1.

Hata hivyo, United ilikuwa na malengo mengine ya kiungo kwa dirisha la majira ya joto ya 2026. Amorim alitaka nyongeza ya kikosi katika dirisha la Januari ili kuongeza nafasi ya Man United kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Lakini, timu nyingi zimekuwa zikikwepa kufanya usajili mkubwa dirisha la Januari.

Man United kwa sasa ipo nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, pointi tatu tu nyuma ya timu inayoshika nafasi ya nne, Liverpool na tayari ligi hiyo imeshuhudiwa mechi 21.

Kutokana na hilo, kikosi hicho ambacho kwa sasa kipo chini ya kocha wa mpito, Darren Fletcher kinahitaji kugangamala ili kutimiza lengo hilo la kumaliza kwenye nafasi nne za juu zinazotoa tiketi ya moja kwa moja ya kuingia kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.