Mourinho awalaza mastaa mazoezini
Muktasari:
- Miamba hiyo ya Lisbon ilitupwa nje ya nusu fainali ya michuano ya Taca de Liga kutokana na kipigo hicho kizito.
LISBON, URENO: JOSE Mourinho amewataka mastaa wa Benfica kulala kwenye uwanja wa mazoezi baada ya kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Braga.
Miamba hiyo ya Lisbon ilitupwa nje ya nusu fainali ya michuano ya Taca de Liga kutokana na kipigo hicho kizito. Kocha Mourinho alionekana kuchukizwa na suala hilo na kuamua wachezaji hao wabaki kwenye uwanja wa mazoezi wa Seixal, akiamini hawataka muda wa kulala, kwa sababu upo umbali wa maili 10kutoka kwenye uwanja wao wa mechi wa Estadio da Luz.
Mourinho, 62, alidai kwamba wachezaji hao wanapaswa kubaki kwenye uwanja huo wa mazoezi hadi mechi yao ijayo.
Akizungumza baada ya mechi, Mourinho kwa hasira amesema: “Wachezaji watalala Seixal, na Alhamisi watafanya mazoezini na siku moja baadaye kutakuwa na mazoezi. Kwa sababu Jumamosi hatuchezi, mechi yetu ijayo tutakawabaliki FC Porto, Jumatano ijayo.
“Tutakapowasili Seixal, kila mtu atakwenda kwenye chumba chake. Nadhani wachezaji watalala vizuri kama ambavyo mimi nitalala, nikiwa na maana kwamba hawatakuwa na usingizi. Hicho ndicho ninachotaka, wasilala na badala yake wawaze sana, kitu gani nitakifanya.”
Baada ya Benfica kupoteza nafasi za kufunga mapema kabisa katika mechi hiyo, Braga wakafanya kweli na kupata bao la kuongoza uwanjani Estadio Dr Magalhaes Pessoa katika dakika 18. Pau Victor ndiye aliyefunga bao hilo kabla ya Rodrigo Zalazar kuongeza jingine na kwenda mapumziko wakiwa 2-0.
Kikosi cha Mourinho kilipata matumaini dakika 64, wakati staa Vangelis Pavlidis alipofunga kwa mkwaju wa penalti. Lakini, Braga ilirejesha uongozi wake wa tofauti wa mabao mawili katika dakia 10 za mwisho, wakati beki wa zamani wa Celtic, Gustaf Lagerbielke aliposukumia mpira nyavuni. Mambo yalizidi kuwa mabaya zaidi kwa Benfica baada ya kumpoteza beki wao wa kati, Nicolas Otamendi kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa njano mbili. Mourinho alirudi kuinoa Benfica, Septemba mwaka jana ikiwa ni wiki moja tu tangu alipofutwa kazi Fenerbahce.