Amorim achukua kiti cha Ten Hag Man United

Muktasari:
- Amorim ametangazwa kuchukuwa nafasi hiyo, akisaini mkataba wa miaka mitatu ambao utafikia kikomo Juni 2027, huku akiwa na chaguo ka kusaini mkataba mpya, endapo atafikia malengo ya klabu hiyo ya Old Trafford.
Uongozi wa klabu ya Manchester United umemtangaza Ruben Amorim kuwa kocha mkuu, akichukua nafasi ya Erik Ten Hag ambaye alisitishiwa mkataba wake mwanzonin mwa wiki hii.
Amorim ametangazwa kuchukuwa nafasi hiyo, akisaini mkataba wa miaka mitatu ambao utafikia kikomo Juni 2027, huku akiwa na chaguo ka kusaini mkataba mpya, endapo atafikia malengo ya klabu hiyo ya Old Trafford.
Hata hivyo, kocha huyo kutoka nchini Ureno hatokuwa sehemu ya benchi la ufundi la Man United katika mchezo wa keshokutwa Jumapili dhidi ya Chelsea, hivyo Ruud van Nistelrooy ataendelea kuinoa timu hiyo.
Taarifa ya Man United inaeleza kuwa Amorim ataanza kazi rasmi klabuni hapo Jumatatu, Novemba 11.
Ruben ni mmoja wa makocha wachanga wenye kusisimua na wenye viwango vya juu katika soka la Ulaya. Akiwa amepambwa sana kama mchezaji na kocha, huku akishinda mataji ya Ligi Kuu mara mbili nchini Ureno akiwa na Sporting CP.