Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yaongeza mzigo kwa Mbeumo

MBUEMO Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa, Brentford inahitaji dau la zaidi ya Pauni 60 milioni kwa ajili ya kumuuza na ilikataa ofa ya kwanza ya Mashetani Wekundu kwa sababu ilikuwa ndogo.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inapanga kutuma ofa mpya kwenda Brentford kwa ajili ya straika wa timu hiyo Bryan Mbeumo baada ya ile ya kwanza ya Pauni 55 milioni kukataliwa.

Inaelezwa, Brentford inahitaji dau la zaidi ya Pauni 60 milioni kwa ajili ya kumuuza na ilikataa ofa ya kwanza ya Mashetani Wekundu kwa sababu ilikuwa ndogo.

United iliwasilisha ofa ya Pauni 45 milioni na nyongeza ya Pauni 10 milioni kama bonasi ya awali.

Mbeumo, mwenye umri wa miaka 25, ni miongoni mwa wachezaji wanaopewa kipaumbele na Man United katika mpango wa kuboresha kikosi chao kilichoshindwa kufanya vizuri msimu uliopita.

Man United ilifunga jumla ya mabao 44 tu katika Ligi Kuu, idadi ya pili ya chini zaidi kwa timu ambazo hazikushuka daraja.

Nyota huyo wa Cameroon ambaye mkataba wake unamalizika mwakani na  Brentford wana chaguo la kuongezea mwaka mmoja kwa mujibu wa kipengele kilichpo, anaweza kuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Man United katika majira haya ya kiangazi, baada ya Matheus Cunha aliyesajiliwa kwa pauni  62.5 milioni.

Licha ya kukosa mapato ya Pauni 100 milioni baada ya kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kichapo dhidi ya Tottenham kwenye fainali ya Europa League, Man United inaweza kuongeza fungu la matumizi kupitia mauzo ya wachezaji wa akademi kama Marcus Rashford na Alejandro Garnacho, ambao mauzo yao yatahesabika kama faida kamili chini ya sheria za usawa wa matumizi ya fedha.


Mbeumo amefurahia msimu bora akihusika katika mabao 28 kwenye mechi 38 za EPL akifunga mabao 20 na kutoa asisti 8.

Mwenyewe alionyesha nia ya kujiunga na Man United, jambo lililoripotiwa na Mail Sport siku ya Jumatatu.

Kocha wa Brentford, Thomas Frank, alisema kuwa iwapo Mbeumo atauzwa, basi ni lazima iwe kwa “kiasi kikubwa sana.”

“Kama atauzwa, basi ni kwa kiasi kikubwa. Haiwezekani kumpata mbadala wake kirahisi. Kuna sababu kwa nini anagharimu kiasi hicho, na sisi hatuna fedha hizo za kumsajili mchezaji wa kiwango hicho ikiwa ataondoka, hivyo lazima tufidie.”

Mbeumo alijiunga na Brentford akitokea Troyes ya Ufaransa mwaka 2019, na tangu hapo ameifungia timu hiyo mabao 70 na kutoa asisti 51. Aliisaidia Brentford kupanda daraja mwaka 2021.