Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ALONSO: Dili la Madrid litakavyomtajirisha

ATM Pict

Muktasari:

  • Alonso ambaye kwa sasa anakunja mshahara wa Euro  6 milioni kwa msimu, ikiwa atafanikiwa kujiunga na Madrid anatarajiwa kukunja mshahara wa zaidi ya Euro 10 milioni kwa msimu, kiasi ambacho kitazidi kumfanya kuwa tajiri zaidi mbali ya utajiri alionao kwa sasa.

MADRID, HISPANIA: BAADA ya timu nyingi kuhitaji huduma yake dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana na kuzikataa, Xabi Alonso anayeifundisha Bayer Leverkusen kwa sasa, inadaiwa yuko katika makubaliano na Real Madrid anayoweza kujiunga nayo mara baada ya msimu huu kumalizika ili kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti.

Alonso ambaye kwa sasa analipwa mshahara wa Euro  6 milioni kwa msimu, ikiwa atajiunga na Madrid anatarajiwa kulipwa mshahara wa zaidi ya Euro 10 milioni kwa mwaka, kiasi ambacho kitazidi kumfanya kuwa tajiri zaidi.

AT 03

ANAPIGAJE PESA

Mbali ya mshahara wa Euro 6 milioni kwa mwaka anaoupata kwa sasa Bayer Leverkusen, aliwahi pia kulipwa  wakati wa uchezaji wake na pesa nyingi zaidi aliipata akiwa na Bayern Munich alikokuwa analipwa Dola 13 milioni kwa mwaka.

Mbali na mishahara aliyowahi kupokea na anayopokea, Alonso anapata pesa za kutosha kutokana na bonasi na madili mengine ya kuwa balozi wa kampuni mbalimbali.

Kwanza kabisa ni balozi wa Adidas iliyokuwa ikimvalisha viatu wakati anacheza na kwa sasa amekuwa akionekana katika matangazo mbalimbali ya kampuni hiyo.

Pia amekuwa akipata pesa nyingine kutokana na miradi yake binafsi na taarifa zinaeleza anamiliki hisa katika kampuni mbalimbali na ana hoteli Hispania zinazomwingizia kipato.

Kijumla anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 20 milioni.

AT 04

MSAADA KWA JAMII

Amewahi kucheza mechi mbalimbali za kirafiki zinazohusisha wacheji wa zamani wa Liverpool na mapato yake huwa yanakwenda kusaidia jamii kwenye vituo vya watoto yatima na watu wenye ulemavu.

Pia amekuwa akishirikiana na taasisi mbalimbali kutoa misaada kwa jamii ikiwa pamoja na Aladina Foundation na mwaka jana aliandaa mchezo wa kirafiki dhidi ya  Real Sociedad na pesa zilizopatikana zilitumika kusaidia taasisi ya Columbus.

AT 01

MJENGO

Ana mjengo wa kifahari maeneo ya San Sebastian, Hispania ambao alimaliza kuijenga  mwaka 2022, inaelezwa nyumba hiyo ina thamani ya Pauni 4 milioni.

Mwaka juzi mamlaka za Hispania zilimtaka kuibomoa kwa sababu haifuati sheria za masuala ya mazingira za nchi hiyo.


NDINGA

Ana ndinga mbalimbali kama Sport SS17, Mercedes 190 SL na Porsche 911 GT3.

Hata hivyo, sio shabiki mkubwa wa magari ya kifahari na kijumla zinakadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 1 milioni. Asilimia kubwa ya pesa zake nyingi ameziwekeza katika biashara mbalimbali.

AT 02

MAISHA NA BATA

Yupo katika ndoa na mrembo Nagore Aranburu tangu mwaka 2009. Alikutana naye akiwa bado kijana mdogo wakati huo alipokuwa anaichezea Real Sociedad.

Kwa pamoja wamepata watoto watatu ambao ni Jontxu Aramburu, Ane na Emma.

Jamaa sio mtu wa bata sana na muda mwingi wa mapumziko huutumia kukaa na familia yake na hata nyakati ambazo huonekana kumbi ama maeneo ya starehe basi pembeni yake huwa na mkewe.