Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot aachiwa Florian Wirtz mwenyewe tu

SLOT Pict

Muktasari:

  • Man City iliripotiwa kuwa mstari wa mbele kwenye kufukuzia saini ya staa huyo wa Bayer Leverkusen, lakini sasa imejiweka kando na kuipa nguvu Liverpool kutumia fursa.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amepata nguvu mpya kwenye msako wao wa kumnasa kiungo mshambuliaji, Florian Wirtz baada ya Manchester City kujiondoa kwenye mchakato huo.

Man City iliripotiwa kuwa mstari wa mbele kwenye kufukuzia saini ya staa huyo wa Bayer Leverkusen, lakini sasa imejiweka kando na kuipa nguvu Liverpool kutumia fursa.

Miamba hiyo ya Ligi Kuu England kwa muda mrefu imekuwa ikimfukuzia kiungo huyo wa Ujerumani aje kukipiga kwenye vikosi vyao.

Bayer Leverkusen inataka kuchangisha Pauni 126 milioni kwenye mauzo ya wachezaji dirisha hili, lakini staa huyo anaweza kupatikana kwa gharama ndogo.

Hata hivyo, bei anayouzwa Wirtz kutokana na masharti ya mikataba iliyowekwa ndicho kitu kilichowafanya Man City kujiweka pembeni na kufikiria kusajili wachezaji wengine.

Man City ilipiga hesabu na kuona mchezaji huyo mmoja anaweza kuwagharimu hadi Pauni 250 milioni kwenye mambo yote kuanzia mishahara na bonasi kwa muda wa mkataba wake.

Kingine pia Wirtz kwa muda mrefu amekuwa akidhaniwa atakuwa tayari kujiunga na Bayern Munich ili abaki kwenye Bundesliga kuliko kwenda nje, lakini mabingwa hao wa Ujerumani, wameweka pembeni mipango yao ya kumsajili.

Huko nyuma Man City iliwahi kuwahitaji mastaa kama Fred, Jorginho, Frenkie de Jong, Harry Kane, Harry Maguire na Kalidou Koulibaly - lakini baadaye ilijiweka pembeni baada ya kuona dili zao zingewagharimu pesa nyingi. Man City kwa sasa inatafuta mchezaji wa kuja kurithi buti za kiungo Kevin De Bruyne na sasa imeelekeza nguvu kwa staa wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White huku ikiamini kinda Claudio Echeverri - naye anaweza kuziba pengo msimu ujao.