Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aguero amtuma mabao Haaland

Muktasari:

  • Haaland, ambaye amefunga mabao 119 katika misimu yake mitatu tangu alipojiunga na Man City, tayari ameshakaribia nusu ya mabao ya Aguero 260, ambayo alifunga kwa miaka 10 aliyodumu katika kikosi hicho cha Etihad.

MANCHESTER, ENGLAND: SUPASTAA, Sergio Aguero anamtaka mtambo wa mabao Erling Haaland kurudi kwenye ubora wake huko Manchester City - afunge mabao ya kutosha kuvunja rekodi yake.

Haaland, ambaye amefunga mabao 119 katika misimu yake mitatu tangu alipojiunga na Man City, tayari ameshakaribia nusu ya mabao ya Aguero 260, ambayo alifunga kwa miaka 10 aliyodumu katika kikosi hicho cha Etihad.

Mabao bado yanapatikana kwa Haaland licha ya kikosi hicho cha kocha Pep Guardiola kupitia nyakati ngumu uwanjani.

Man City ipo kwenye vita kali kutafuta tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na itashuka hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi endapo kama Newcastle United itashinda kiporo chake.

Na straika Aguero - ambaye alistaafu mwishoni mwa mwaka 2021 baada ya kupimwa na kugundulika kuwa na tatizo la moyo wakati alipokuwa akikipiga Barcelona - anaamini Haaland atabaki Man City hadi mwisho wa mkataba wake 2034 na kufanikiwa kuvunja rekodi yake ya mabao kwenye kikosi hicho.

Alipoulizwa kama anahisi Haaland atavunja rekodi yake ya mabao, Aguero alisema: Naamini hivyo! Ni mchezaji mahiri na anakaribia. Nadhani ni yeye atakayeweza kuifikia.”