Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Trent hajaitwa Lions, ila acheze pale mbele’

Muktasari:

  • England itaanza safari ya kusaka taji la Kombe la Dunia ambalo imekuwa ikitamani kulibeba kwa muda mrefu ndani ya siku zisizozidi 70 swali kubwa linalosubiri jibu ni nani anapaswa kuanza katika kikosi hicho Thomas Tuchel watakapokutana na Croatia Juni 17?

LONDON, ENGLAND: BEKI wa kulia wa Real Madrid, Trent Alexander-Arnold ametajwa kwamba anafaa kuwa katika nafasi ya ushambuliaji ya kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England (The Lions) kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

England itaanza safari ya kusaka taji la Kombe la Dunia ambalo imekuwa ikitamani kulibeba kwa muda mrefu ndani ya siku zisizozidi 70 swali kubwa linalosubiri jibu ni nani anapaswa kuanza katika kikosi hicho Thomas Tuchel watakapokutana na Croatia Juni 17?

talkSPORT imechagua kikosi bora zaidi ikizingatia kuwa wachezaji wote wako fiti na mashabiki wa England wanatamani kuona mwaka huu ukiwa ndio ambao hawapaswi kupoteza fursa ya kuvuta ubingwa nyumbani.

Katika kipindi hiki cha kalenda ya Fifa, England inapaswa kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Uruguay na Japan kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Dunia, ambapo kocha Tuchel amechagua kikosi cha wachezaji 35 ambacho kitagawanywa katika makundi mawili ili kupata matokeo bora kutoka kwenye kambi.

Harry Kane, Jude Bellingham na Marc Guehi ni miongoni mwa wachezaji waliopo na uteuzi huo unaweza kutoa taswira ya kikosi cha mwisho cha wachezaji 26 kitakachokwenda kwenye mashindano.

Wachambuzi wa talkSPORT Sam Matterface, Adrian Durham, Danny Murphy na Gabby Agbonlahor wametaja kikosi cha England kwa ajili ya fainali hizo kinachohusisha mabeki wa kati Ezri Konsa na Marc Guehi, huku Reece James na Nico O’Reilly wakicheza pembeni.

Pia wamewavuta kikosini Elliot Anderson kama kiungo mkabaji, huku Jude Bellingham na Declan Rice wakicheza mbele kidogo. Bukayo Saka na Anthony Gordon ni washambuliaji wa pembeni, ilhali Harry Kane akiongoza safu ya ushambuliaji.

Vilevile kuna kikosi kingine kinachohusisha Lewis Hall kama beki wa kushoto, huku safu ya kiungo ikiwa na Elliot Anderson, Declan Rice na Jude Bellingham. Lakini kinachovutia zaidi ni safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Harry Kane akiwa mbele, Marcus Rashford kushoto na Trent Alexander-Arnold kulia. Hii ni hoja mpya, kwani wengi wamekuwa wakijadili Alexander-Arnold anapaswa kucheza beki wa kulia au kiungo. Agbonlahor amemtaja kwa msisitizo Harry Maguire na Morgan Rogers.