Zlatan: Mimi ni rais, kocha na mchezaji

Muktasari:
Ibrahimovic alirejea AC Milan ambako aliwahi kutwaa ubingwa wa Serie A mwaka 2011 akiwa mchezaji huru wakati wa dirisha la usajili la Januari baada ya mkataba wake wa kuichezea LA Galaxy ya Marekani kumalizika.
Milan, Italia. Baada ya kuiongoza AC Milan kuitandika Juventus ikiwa na Cristiano Ronaldo kwa mabao 4-2, Zlatan Ibrahimovic amesema ni wazi klabu hiyo, ingetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Italia 'Serie A' kama ingemsajili mwanzoni mwa msimu.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 38, ameonekana bado kuwa na makali katika michezo mikubwa baada ya kufunga na kutoa assisti wakati AC Milan ikiizamishaJuventus kwenye uwanja wa San Siro jana
Nyota huyo wa Sweden alisema kuwa iwapo angejiunga mapema na AC Milan timu hiyo ingeweza kutwaa taji la Ligi Kuu Italia 'Scudetto' Kama ningekuwa hapa tangu msimu ukianza nadhani ningeshinda Scudetto
Kuna mambo yapo tu, huwezi kuzuia. Ibrahimovic ni mfano mzuri kwa vijana wa Milan ambao ni wachezaji wenzake. Mimi ni rais, kocha na mchezaji, lakini wananilipa kama mchezaji," alisema Ibrahimovic.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa la Sweden mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu licha ya mchango wake katika kikosi hicho hijafahamika kama ataendelea kusalia AC Milan au la.
Sababu za hatima ya Zlatan ndani ya AC Milan kutoamriwa mapema zimetajwa ni kusubiria mipango ya kocha mpya Ralf Rangnick ambaye atainoa timu hiyo msimu ujao kuchukua nafasi ya Stefano Pioli.
Hata hivyo, Ibrahimovic mwenyewe amesema kuwa ndani ya muda mfupi ujao kila kitu kitajulikana juu ya hatima yake. "Kuna miezi michache mbele, ngoja tuone," alisema Ibrahimovic