Young Dee, TMK wakiwasha kwa Mkapa

Saturday September 25 2021
kiduchu pic2
By Ramadhan Elias

WASANI wa Bongofleva Young Dee na kundi la TMK Wanaume likiongozwa na Juma Nature, Temba na KR Mura wamepiga shoo za kibabe ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuwarusha mashabiki wa Simba na Yanga waliopo uwanjani hapa.

Young Dee ndiye alianza kupiga shoo na kuwafanya mashabiki wa Simba na Yanga waliopo uwanjani hapa wainuke kushangilia na kuimba naye nyimbo zake.

Mashabiki hao ambao sio wengi kama ilivyozoeleka zikikutana timu hizo mbili vigogo wa Soka la Tanzania wapo uwanjani kusubiri mtanange wa Ngao ya Hisani utakaozikutanisha Simba na Yanga kuanza saa 11:00 jioni.

Baada ya Dee kupiga shoo ya maana kwa dakika kama 10 hivi, waliingia TMK Wanaume na kuliamsha kama kawaida yao huku ngoma za Mugambo na Nampenda Yeye zikionekana kupendwa zaidi.

TMK wamepiga shoo kwa dakika zisizozidi 15 kisha kuondoka huku mashabiki wakiendelea kuwashangilia.

Katika mechi ya leo, Simba ndio wenyeji wakiwa wametwaa Ngao ya Jamii mara Sita huku watani zao Yanga wakiwa wamebeba mara tano kwa misimu tofauti tofauti.

Advertisement
Advertisement