Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yawavuruga maafande

Muktasari:

Yanga imefanikiwa kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikiongoza kwa mabao mawili dhidi ya maafande JKT Tanzania katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Yanga imefanikiwa kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikiongoza kwa mabao mawili dhidi ya maafande JKT Tanzania katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mabao ya Yacouba Songne na Tuisila Kisinda, yametosha kuifanya Yanga iwe mbele na kuwa na mguu mmoja mbele kwenye kuibuka na ushindi leo.

Mabao hayo yamewafanya mashabiki wa timu hiyo waliopo uwanjani waamini kazi imekwisha licha ya kuwepo kwa dakika nyingine 45 za kipindi cha pili.

Kauli ya dalili njema huonekana mapema Asubuhi, inawezekana ikafanya kazi kwa Yanga leo kutokana na ukweli wa kwamba, wamefanikiwa kuwadhibiti vilivyo JKT Tanzania.

Licha ya kupiga kona tatu, maafande hao wameshindwa kabisa kuwa na madhara kwa Yanga, mipira yao ikishindwa kupenya kila wakikaribia eneo la hatari la Yanga.

Ni shambulizi moja pekee la hatari walilofanikiwa kupata JKT ambalo lilikuwa la Danny Lyanga, aliyekaribia kufunga kwa shuti kali lakini likaokolewa na kipa Metacha Mnata

Imeandikwa na Matereka Jalilu