Yanga yaiondoa Ken Gold Kombe la Azam

Mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) uliozikutanisha timu za Yanga na Ken Gold kutoka ya Chunya mkoani Mbeya umemalizika kwenye uwanja wa Uhuru huku Yanga ikiibuka na ushindiwa bao 1-0.

Bao hilo pekee la Yanga lilifungwa dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza na straika wa Yanga Fiston Abdulrazak  raia wa Burundi kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Ken Gold , Boniface Mwanjonde kushika mpira ndani ya 18 akiwa katika harakati za kuokoa hatari za washambuliaji wa Wanajangwani.

Pamoja na kwamba Ken Gold iliibania Yanga kupata bao baada ya mapumziko, lakini mpira uliofika mikononi mwa kipa Farouk Shikalo ni mara moja kipindi chote cha pili.

Dakika ya 78 Notkely Masasi alipiga shuti ambalo lililenga moja kwa moja langoni kwa Shikalo na akadaka kwa kipindi chote cha pili.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu hizo, ingawa Yanga ndio ilifika mara nyingi langoni kwa Ken Gold.

Yanga ilicheza kwa mbinu zaidi tofauti na kipindi cha kwanza ambacho licha ya kupata bao la kuongoza dakika ya 40 safu yao ya mbele haikuwa makini katika umaliziaji.

Kocha wa timu hiyo, Cedric Kaze alifanya mabadiliko dakika ya 59 alimtoa Deus Kaseke na nafasi yake ilichukuliwa na Haruna Niyonzima ambaye aliisaidia timu kutengeneza mashambulizi zaidi.

Badae Kaze alifanya mabadiliko mengine alimtoa Ditram Nchimbi dakika ya 66 na aliingia Carlos Carlhinos ambaye dakika ya 67 alinusura afunge bao.

Ilikuwa hivi mpira ulitoka kwa Niyonzima alimpasia Farid Mussa ambaye alipiga ndani ya 18 ya mlinda mlango wa Ken Gold, Adam John na Carlhinos aliiunga kwa kichwa na kipa akawa makini akaudaka.

Dakika ya 78 Notkely Masasi alipiga shuti la kwanza lililofika mikononi mwa kipa wa Yanga, Farouk Shikalo.

Dakika 82 Carlhinos alipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga ngumu ya kiungo Boniface Mwanjonde, akiwa amekaa uwanjani dakika 16 aliingia dakika ya 66.

Dakika 90 za kipindi cha pili zilimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 dakika 40 za kipindi cha kwanza.

Mashabiki hawajafurahia ushindi?

Imezoeleka kuona amshaamsha za mashabiki wa Yanga timu inaposhinda, leo imekuwa tofauati kwenye mechi hiyo.

Pamoja na Wanajangwani hao kuibuka na ushindi lakini baada ya dakika 90 mashabiki walionekana kutawaliwa na mjadala wa kutokukubaliana na uwezo wa kiwango kilichoonyeshwa na timu yao.

Mashabiki wa Yanga, baadhi walitoka na wengine kubaki uwanjani bila amshaamsha za kuishangilia timu yao kubaki kwenye Kombe la Shirikisho la Azam.

Kama haitoshi baadhi ya wachezaji wa Yanga wakati wanatoka uwanjani wakati wanaionyesha ishara ya kupiga makofi kwa mashabiki hawakuonyeshwa mwitikio kama ilivyozoeleka kupokewa kwa shangwe la kutosha.