Fiston aitanguliza Yanga Uhuru

Yanga imetoka kifua mbele kwa kuongoza bao 1-0 dakika 45 za kipindi cha kwanza dhidi ya Ken Gold kutoka Chunya.

Tukio la Yanga kupata penalti lilitokana na beki Boniface Mwanjonde kushika mpira ndani ya 18 akiwa katika harakati za kuokoa hatari za washambuliaji wa Wanajangwani, ambapo mwamuzi Hamed Arajiga kutoka Manyara aliamua ipigwe penalti.

Straika wa Yanga, Fiston Abdul raia wa Burundi alipiga penalti hiyo na kuipa Yanga bao la kuongoza dakika ya 40.

DAKIKA 15 ZA KWANZA

Dakika 15 za mwanzo Yanga imeanza kwa kasi lakini umakini ulikosekana katika umaliziaji.

Ambapo straika Ditram Nchimbi ameonekana kujituma lakini amejikuta juhudi zake zimegonga mwamba licha ya kukamia kutaka kufunga

Kadri muda ilivyokuwa unayoyoma ndivyo Yanga ilizidi kupata upinzani wa kufungiwa njia ya kwenda mbele kufunga hadi ilivyopatikana penalti dakika ya 40.

Hata hivyo Mwanaspoti limewachambua baadhi mastaa wa Yanga walichokifanya ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.

MAKAPU VS MWAMNYETO

Nahodha msaidizi wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto ndiye anayebaki zaidi eneo la kati, huku akimuacha Said Makapu apande kumsaidia Paul Godfrey.

Wameimalisha eneo la ulinzi ingawa washambuliaji wa timu Ken Gold kutoka Chunya,wanaonekana kukosa malengo ya kutengeneza nafasi za kufunga.

KASEKE VS NCHIMBI

Winga Deus Kaseke ambaye mashabiki wamesikika wakimuita 'Mwaisa' anatumia nguvu zaidi kufosi mashambulizi kutokana na maumbo ya mabeki wa Ken Gold kuwa makubwa na wanatumia nguvu.

Wakati huo huo mshambuliaji wa Ditram Nchimbi ameonekana kupambana kutumia nguvu kubwa lakini umaliziaji wake unakuwa hauna madhara kwa wapinzani, jambo linalowakera mashabiki wanaofuatilia mchezo huo.

MAUYA VS FEI TOTO

Eneo la kati ambalo kuna Zawadi Mauya na Fei Toto, wameonekana wakifanya kazi yao kwa umakini wakusaidiana na mabeki kukaba pia kupeleka mashambulizi kwa wakati.

Fei Toto amejaribu kupanda juu mara kea mara kuisaidia timu kusaka bao, kipindi cha kwanza Yanga ikipambana kusaka ushindi.