Yanga yabanwa mbavu Dodoma

LICHA ya kuingia kwa wachezaji nyota wa Yanga, bado haikusaidia timu hiyo kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa mwisho.
Feisal Salum, Yacouba Songne na Tuisila Kisinda, waliingizwa kipindi cha pili ili kuongeza nguvu kwa Yanga, ili kujaribu kufunga bao lakini haikusaidia.
Nyota hao ambao wamekuwa na ubora uliowafanya kujihakikishia nafasi ya kuanza kwa Yanga, waliingia badala ya Saido Ntibazonkiza, Wazir Junior na Deus Kaseke.
Upande wa Dodoma Jiji, kocha Mbwana Makata, alifanya mabadiliko ya kuwatoa, Mcha Khamis, Enrick Nkosi na Dickson Ambundo, nafasi zao wakiingia Seif Karihe, Omary Daga na Rajab Mgalula.
Matokeo hayo, yameifanya Dodoma Jiji ifikishe alama 44 wakati Yanga imemaliza na alama 74 kwenye nafasi ya pili.