Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Camara wa Berkane adai Simba ina timu nzuri, lakini...

Muktasari:

  • Camara ambaye ni raia wa Senegal, amesema wanaiheshimu Simba kama timu kubwa barani Afrika lakini wamekuja Zanzibar wakiwa na dhamira moja kuhakikisha wananyakua taji la tatu la Kombe la Shirikisho Afrika.

KIUNGO wa RS Berkane, Mamadou Lamine Camara, amesema licha ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika fainali ya mkondo wa kwanza dhidi ya Simba SC huko Morocco, lakini hawatarajii mechi nyepesi kesho Jumapili kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Camara ambaye ni raia wa Senegal, amesema wanaiheshimu Simba kama timu kubwa barani Afrika lakini wamekuja Zanzibar wakiwa na dhamira moja kuhakikisha wananyakua taji la tatu la Kombe la Shirikisho Afrika.

“Hatujui kama itakuwa rahisi dhidi ya Simba ambayo ni timu nzuri sana. Tupo hapa tukitambua kile kinachotukabili. Tupo kwa ajili ya mechi ya furaha, fainali ni muda wa historia,” amesema Camara.

Katika mechi ya kwanza iliyofanyika wikiendi iliyopita nchini Morocco, mabao ya Camara na Oussama Lamlaoui yaliipa Berkane ushindi wa 2-0.

Hata hivyo, Camara anaamini nafasi walizopoteza katika mechi hiyo ni jambo walilolifanyia kazi ili kuhakikisha hawapotezi ufanisi tena.

“Tulisema hatukufurahishwa sana kwa sababu tulikosa ufanisi. Tulipaswa kushinda zaidi. Lakini muhimu zaidi ni kwamba baada ya mechi ile, tumepata mafunzo mengi. Tumefanyia kazi hilo ili tusirudie makosa katika mechi ya kesho,” amesema.

Camara pia aliweka wazi kuwa kwa sasa hafikirii chochote kuhusu mustakabali wake wa baadaye kwa sababu ana mkataba na RS Berkane na anafurahia maisha ndani ya klabu hiyo.

“Kwa sasa nina mkataba na Berkane. Nina furaha, niko vizuri hapa. Kwa sasa siwezi kuzungumzia siku za baadaye, akili yangu yote ipo kwenye fainali hii ambayo ni muhimu sana kwetu. Baada ya hapo, tutaona,” amebainisha kiungo huyo raia wa Senegal.