Yanga yaandika historia CAFCL, Pacome aiteka shoo

Baada ya kufuta gundu la miaka 25 kutinga hatua ya makundi, Yanga imeweka historia leo baada ya kufuzu hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza.

Yanga imetinga hatua hiyo baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria  na kinachoibeba ni matokeo mazuri katika mechi baina yao.

Ilikuwa ni shoo ya Pacome Zouzoua ambaye ilikuwa ni siku yake iliyopewa jina la 'Pacome Day'  na ameonyesha kiwango kikubwa kwenye mchezo huo akiwapa raha mashabiki wao ikiwamo kutoa asisti ya bao la tatu alilofunga Kennedy Musonda.

Mabao ya Mudathir Yahya, Aziz KI, Musonda na Joseph Guide yamepeleka shangwe kwa mashabiki waliofurika kuishangilia timu hiyo iliyokuwa na 'Shoo ya Pacome' kama ilivyoandaliwa na uongozi wa timu hiyo.

Yanga ndiyo timu ya kwanza kuifunga timu za Waarabu mabao mengi (4-0) ikifanya hivyo leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku pia ikiwa ndiyo timu iliyofunga mabao mengi kwenye hatua ya makundi ikiwa ni raundi ya tano.

Katika hatua nyingi, Mabingwa hao watetezi wa Ligi Ku8u Bara imeiachia msala watani zao wa jadi, Simba ambayo ilitoka suluhu dhidi ya Asec Mimosas jana Ijumaa na inahitaji ushindi (pointi tatu) ili kujihakikishia kufuzu robo fainali ya Caf CL.

Ynga itakutana na Al Ahly kwenye mchezo wa marudio jijini Cairo, Misri ukiwa ni wa kumaliza hatua ya makundi kabla ya kaunza kwa hatua ya robo fainali.