Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKILI ZA KIJIWENI: Yanga haimdai chochote Hamdi

HAMDI Pict

Muktasari:

  • Kwa sisi hapa kijiweni kwetu hatufahamu nini kitaendelea kwa Kocha Miloud Hamdi wa Yanga ambaye muda huo atakuwa ameinoa timu hiyo kwa miezi sita tu.

MSIMU utamalizika Juni baada ya mabadiliko ya ratiba yaliyofanywa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) hivi karibuni na mechi za mwisho za Ligi Kuu zitachezwa Juni 22.

Kwa sisi hapa kijiweni kwetu hatufahamu nini kitaendelea kwa Kocha Miloud Hamdi wa Yanga ambaye muda huo atakuwa ameinoa timu hiyo kwa miezi sita tu.

Labda Yanga inaweza kuamua kuachana naye kama ambavyo tetesi za hapa na pale zimekuwa zikidai au ikaamua kuendelea naye kwa muda mrefu zaidi.

Kwa uamuzi wowote ambao Yanga itaamua kuuchukua kwa kocha huyo mwishoni mwa msimu, kijiwe kimekubaliana kwa kauli moja Hamdi hana anachodaiwa na timu hiyo kutokana na kile ambacho amekifanya hadi sasa.

Aliikuta timu inafanya vizuri katika Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la TFF na akafanikiwa kuendeleza ubora wa matokeo lakini hata kiwango cha uwanjani kama ambavyo aliikuta kutoka kwa kocha aliyemtangulia, Sead Ramovic.

Zile dozi dozi ambazo Yanga ilikuwa inazitoa chini ya Miguel Gamondi na Ramovic ameziendeleza huku timu ikiendelea kuwa na safu imara ya ulinzi ambayo imekuwa hairuhusu mabao kirahisi katika mashindano tofauti.

Kitu kingine ambacho nakiona Hamdi amefanikiwa nacho ni kujitahidi kutoa nafasi ya kucheza kwa idadi kubwa ya wachezaji wake tofauti na watangulizi wake ambao walionekana kuwa na imani na wachezaji wachache na wengine wakiwasotesha benchi.

Kocha anayetoa nafasi ya kucheza kwa kundi kubwa la wachezaji ni rahisi kufanikiwa kwa vile vijana wake watajitahidi wasimuangushe kwa kuhakikisha timu inafanya vizuri ili aendelee kubakia.

Kama ni mtoto alipewa kulea, Hamdi amemlea vizuri na kiufupi hata ikitokea anaondoka leo, hatokuwa na baya kwa watu wa Yanga. Katumikia vyema nafasi yake.