Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maabad aukubali mziki wa Mzize

MAABAD pict

Muktasari:

  • Alisema Mzize amekuwa na mwendelezo mzuri na msimu uliopita alifunga mabao sita na asisti saba katika mechi 29 alizocheza sawa na dakika 1,299, huku msimu huu akiwa na mabao 13 na asisti nne akicheza mechi 26 kwa dakika 1,597.

MSHAMBULIAJI wa Coastal Union, Maabad Maulid Maabad amesema kwa msimu huu mshambuliaji Clement Mzize ndiye mzawa aliyemvutia zaidi kutokana na kiwango alichoonyesha kuisaidia Yanga.

Alisema Mzize amekuwa na mwendelezo mzuri na msimu uliopita alifunga mabao sita na asisti saba katika mechi 29 alizocheza sawa na dakika 1,299, huku msimu huu akiwa na mabao 13 na asisti nne akicheza mechi 26 kwa dakika 1,597.

Maabad alisema anaamini Mzize akilinda kiwango alichonacho atakuwa kama John Bocco aliyewahi kucheza Azam, Simba na sasa JKT Tanzania.

“Bocco ndiye mzawa aliyekuwa na muendelezo wa kufunga mabao kila msimu, ndicho ninachokiona kwa Mzize, naamini akitunza kiwango chake akiwa na washauri wazuri wanaomzunguka atakuwa mzawa anayetegemewa Taifa Stars,” alisema Maabad na kuongeza. “Mfano anavyoimbwa Prince Dube mwenye mabao 12, angekuwa anaimbwa hivyo Mzize umaarufu wake ungekuwa mkubwa zaidi.”

Wachezaji wengine wanaomvutia Maabad ni Herness Malonga wa Singida Black Stars na Ibrahim Ame wa Mashujaa anaowaona wana vipaji vikubwa.

“Ujue kuna timu ambazo wachezaji ni rahisi sana kuonekana vipaji vyao ama aina ya uchezaji wao, lakini Ame na Malonga nimekuwa nikiwafuatilia, ni wachezaji wazuri sana,” alisema mshambuliaji huyo ambaye msimu huu kwenye ligi amefunga mabao matano na asisti mbili.

Alisema anachokitarajia katika mechi tatu zilizosalia dhidi ya Tanzania Prisons, Fountain Gate na Tabora United ni kupambana angalau aongeze idadi ya mabao.