Yanga yaalikwa mechi ya kirafiki Malawi

Muktasari:
- Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amezungumza leo na waandishi wa habari nakusema wamepata mwaliko wa mechi ya kirafiki nchini Malawi Julai 6, 2023 dhidi ya Big Bullet
Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amezungumza leo na waandishi wa habari nakusema wamepata mwaliko wa mechi ya kirafiki nchini Malawi Julai 6, 2023 dhidi ya Big Bullets
"Tumepokea mwaliko maalumu kutoka kwa Serikali ya Malawi kucheza mchezo maalumu kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi itakayofanyika Julai 6, 2023. Ni heshima kubwa sana kwa Klabu yetu na kwa Taifa kwa ujumla"
"Siku ya maadhimisho tutacheza na Nyasa Big Bullets ya Malawi na Juai 5 tutakutana na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera"
Ally Kamwe amesema wachezaji wa Yanga watajea kambini julai 10, 2023 kwajili ya 'Pre season' kujiandaa na msimu ujao Ligi Kuu na kimataifa.
"Wachezaji wataanza kuripoti kuanzia Julai 10 kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, wale tulikuwa nao msimu uliopita na tuliowasajili"
"Wachezaji wakishafika kambini ndo tutawatangazia timu itakwenda wapi kama tutabaki Avic Town au nje ya Tanzania"