Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga washerekea pointi tatu na Yatima Arusha

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeamua kusherehekea ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC, na watoto Yatima waishio katika kituo cha Faraja Orphanage kwa kuwapatia msaada wa vyakula mbali mbali.

Yanga ambao ndio vinara wa Ligi Kuu msimu huu, wamefikisha jumla ya alama 40 baada ya kumchapa 3-1 timu ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa juzi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Baada ya ushindi huo, wanachama na mashabiki wa Yanga mkoani hapo walijisachi mifuko yao na kuchanga kiasi cha shilingi milioni moja haraka haraka kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji wao, lakini wachezaji nao wakaamua fedha hiyo iwe sadaka kwa yatima kupata mlo wa kusherehekea sikukuu za Christmas na mwaka mpya zinazotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Akizungumza katika kituo cha Faraja, Ofisa Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema kuwa wamenunua mbuzi watatu, vyakula mbali mbali na matunda Sambamba na vifaa vya usafi na zawadi kwa watoto ambayo wamewakabidhi na pesa taslim kwa ajili ya mahitaji mengine.

"Kwa niaba ya uongozi mzima wa Yanga Taifa na mkoa wa Arusha tumefurahia Sana kupata ushindi huu na tukaazimia kwa pamoja kuungana na Yatima katika furaha hii hasa ya kuwapa mkono wa heri na faraja kuelekea sikukuu za Christmas na mwaka mpya tusherehekee pamoja hivyo naombeni mpokee sadaka hii yetu kwa pamoja," alisema Nugaz akikabidhi misaada hiyo.

Kwa upande wake mmiliki na mlezi mkuu wa kituo hicho cha Faraja Orphanage, Faraja Maliaki alishukuru kwa msaada huo akisema kuwa utakuwa furaha kubwa na ya aina yake kwa watoto hao kupewa uhakika wa chakula msimu huu mzima kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

"Kituo hiki cha faraja chenye watoto 200, tunawapata kupitia mahospitalini wanaotelekezwa, maendeleo ya jamii kwa wale wanaotupwa mitaroni, lakini pia jela za watoto na watu wazima wanaojifugua huko ambao kati yao 30 wameathirika na virusi vya Ukimwi (VVU) na wanatumia dawa," alisema Maliaki

Alisema kuwa changamoto kubwa katika kulelea watoto hao kwa sasa ni uhakika wa chakula hali inayowazimu kushindia mlo mmoja siku zingine Sambamba na mavazi zimechakaa huku mfadhili mkuu aliyekuwa anawasaidia akifariki kwa ugonjwa wa Covid-19, hivyo kuiomba jamii ijitokeze kuwasaidia kupata misaada ya vyakula wakiendelea na utaratibu wa kusaka mfadhili na miradi ya uhakika wa chakula.

Naye mwenyekiti wa Yanga mkoa wa Arusha Felician Mombo alisema kuwa walifikia hatua ya kuchanga fedha hizo zisaidie katika baadhi ya Mambo katika klabu yao lakini wamefurahia uamuzi wa uongozi kuelekeza katika kituo cha watoto Yatima hali ambayo imewapa funzo kubwa lakini pia imeshusha furaha na faraja kwao.