Yanga wapo sawa kuhamia KMC

Muktasari:
- Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda alisema Kanuni ya 9(4) inawapa haki Yanga na timu nyingine ambazo hazina uwanja wake inaoumiliki kuhama kama tu ha-wakuwa na makubaliano na wamiliki.
Wakati Yanga ikitangaza kuhamia KMC Complex kutoka Azam Complex, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa tamko. Awali wakati Yanga ikitangaza kuhama uwanja, Bodi ya Ligi ilibainisha imepokea ombi lao lakini haijalitolea uamuzi.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda alisema Kanuni ya 9(4) inawapa haki Yanga na timu nyingine ambazo hazina uwanja wake inaoumiliki kuhama kama tu ha-wakuwa na makubaliano na wamiliki.
“Ni sawa kwa Yanga kuhama kwani makubaliano yao na Azam yameharibika, japo hatujawapa barua ya kibali ila kikanuni wanaruhusiwa kuhamia uwanja mwingine uliopo ndani ya mkoa huohuo au nje kid-ogo.
“Uwanja watakaohamia uwe umehakikiwa na Bodi ya Ligi kama utafaa kutumika, kwa hivyo ombi lao lina mashiko,” alisema Boimanda.