Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Dodoma Jiji yanukia Zenji

DODOMA Pict

Muktasari:

  • Hatua ya mechi hiyo kupelekwa Zanzibar inaelezwa ni kutokana na Uwanja wa KMC Complex ambao inautumia Yanga kwa mechi za nyumbani kutumiwa na watani zao Simba watakaoikaribisha Kagera Sugar tarehe husika.

MECHI ya Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Dodoma Jiji iliyopangwa Juni 22 huenda ikachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar endapo mambo yataenda kama yalivyopangwa awali.

Hatua ya mechi hiyo kupelekwa Zanzibar inaelezwa ni kutokana na Uwanja wa KMC Complex ambao inautumia Yanga kwa mechi za nyumbani kutumiwa na watani zao Simba watakaoikaribisha Kagera Sugar tarehe husika.

Taarifa kutoka Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), zimelidokeza Mwanaspoti mechi hiyo iko mbioni kupelekwa Zanzibar ikiwa ni siku tatu kabla ya kikosi hicho kurejea Dar es Salaam kucheza na Simba Juni 25 katika pambano la Dabi ya Kariakoo.

Mechi dhidi ya Dodoma Jiji ilikuwa ya mwisho kwa Yanga msimu huu kwenye ligi, lakini sasa ni ya pili kutoka mwisho baada ya kutangazwa Dabi ya Kariakoo itachezwa Juni 15 kutoka Juni 15 iliyotangazwa kufuatia awali Machi 8, 2025 kuota mbawa.

Taarifa zinaeleza Yanga ilipanga kucheza na Dodoma Jiji Juni 22 Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kuweka kambi pia hadi Juni 28 itakapocheza fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Singida Black Stars.

Kitendo cha Yanga kucheza na Simba Juni 25 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, maana yake itaenda Zanzibar kupambana na Dodoma Jiji kisha itarudi Dar kumalizana na Simba na kurejea visiwani humo kukipiga na Singida Black Stars.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga alisema hawana taarifa zozote za mechi hiyo dhidi Yanga kuchezwa Zanzibar, ingawa wanachoendelea nacho kwa sasa ni maandalizi ili kuhakikisha wanamaliza msimu huu vizuri.

“Maandalizi yetu yanaenda vizuri na tumekuwa na mechi nyingi za kirafiki hivi karibuni kwa lengo la kujipima nguvu kabla ya zile za ushindani hazijarejea, japo suala la kucheza Zanzibar na Yanga hilo kwa kweli halijanifikia,” alisema Mpunga.